Simba yaja na 'Is not Over, Kazi Iendelee'

Thursday October 21 2021
simba botswana pic
By Clezencia Tryphone

UONGOZI wa Simba umetangaza viingilio vya mchezo wao wa Jumapili huku wakija na kauli mbiu mpya isemayo 'Is not Over, Kazi Iendelee'.

Simba Jumapili itashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kucheza mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Simba itashuka dimbani ikiwa na mtaji wa mabao 2-0 ambayo waliyapata Nchini Botswana wiki iliyopita yakifungwa na Thadeo Lwanga na John Bocco.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Simba Ally Shatry 'Chiko' amesema viingilio katika mchezo huo mzunguko itakuwa Sh5,000 VIP B na C Sh20, 000 VIP A Sh40, 000 huku Platinumz Sh150, 000.

"Viingilio hivyo kadi zinapatikana mtandaoni na katika maeneo mbalimbali ambayo tiketi zitatangazwa kuuzwa, wanasimba wachangamkie kuja kusapoti vijana wao katika mchezo huo, "amesema Chiko.

Chiko amesema kikosi chao kipo vizuri na tayari kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano ambao utawapa nafasi ya kutinga hatua ya makundi.

Advertisement

Naye, mhamasishaji Mwinjaku amewataka wanasimba kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mkapa kusapoti timu yao.

Katika mchezo huo CAF imewaruhu Simba kuingiza mashabiki 15,000.

Advertisement