Simba yafunika nyota Stars

Muktasari:
Azam yenyewe imetoa nyota wanne ambao ni Agrey Morris, David Mwantika, Mudathir Yahya na Frank Domayo idadi sawa na Yanga.
Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Ligi Ku Tanzania Bara, Simba wameongoza kwa kutoa nyota wengi kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na fainali za Afrika (Afcon).
Katika kikosi cha nyota 39 walioitwa Leo Mei Mosi na kocha Emmanuel Amunike, Simba ndiyo imeongoza kwa kutoa nyota wengi ikifuatiwa na Yanga na Azam.
Nyota wa simba walioitwa kwenye kikosi hicho ni kipa Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude na John Bocco.
Azam yenyewe imetoa nyota wanne ambao ni Agrey Morris, David Mwantika, Mudathir Yahya na Frank Domayo idadi sawa na Yanga.
Katika kikosi cha Afcon, Yanga imetoa pia nyota wanne ambao ni Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Feisal Salum na Ibrahim Ajib.
Timu ya Lipuli imetoa nyota watatu ambao ni Ally Mtoni, Fred Tangalu na Miraji Athuman
Wakati Mbao imetoa nyota wawili ambao ni Metacha Mnata na Vicent Philipo sawa na Tenerife ya Spain ambayo imemtoa Shabani Chilunda, Farid Mussa.
Timu nyingine zilizotoa mchezaji mmoja mmoja ni Malindi (Suleiman Salula), Tanzania Prisons (Aron Kalambo), timu ya vijana ya U20 (Claryo Boniface) na Nkana ya Zambia(Hassan Kessy)
Nyingine ni KMC (Ally Ally), Singida United (Kennedy Wilson), Petrojet ya Misri (Himid Mao), Osmaily ya Misri (Yahya Zaydi), Enppi ya Misri (Shiza Ramadhan) na Difaa El Jadid ya Morocco (Simon Msuva).
Nyingine ni Genk ya Ubelgiji (Mbwana Samatta), JS Saoura Algeria (Thomas Ulimwengu), Coastal Union (Ayoub Lyanga), Kagera Sugar (Kassim Hamis) timu ya U17 (Kelvin John), Solihull Moors ya Uingereza (Adi Yussuf) na Baroka FC ya Afrika Kusini (Abdi Banda)
Timu hiyo itajiandaa na fainali za Afcon zitakazoanza Juni 21 hadi Julai 19 nchini Misri.
Stars imefuzu kucheza Afcon msimu huu kwa kujikusanyia pointi nane katika kundi L baada ya kuifunga Uganda 3-0 kwenye mchezo wa mwisho awali ilisuluhu mjini Kampala. Matokeo mengine iliifunga Cape Verde 2-0 Dar es Salaam, ikafungwa ugenini 3-0, ilitoka suluhu na Lesotho Dar es Salaam, kisha ikafungwa 1-0 mjini Maseru.