Simba watinga bungeni

Muktasari:
- Wachezaji na benchi la ufundi la klabu ya simba nchini Tanzania wametinga bungeni na kushangiliwa na wabunge.
Dodoma. Wabunge wa Bunge la Tanzania wameibuka kwa shangwe kuwashangilia wachezaji na benchi la ufundi la klabu ya Simba.
Wachezaji hao walitinga bungeni leo Jumatano Februari 2, 2021 wakiwa wamevalia sare za klabu yao zenye rangi nyeupe na nyekundu.
Wachezaji hao walitambulishwa bungeni na Naibu Spika Dk Tulia Ackson amesema wachezaji hao ni wageni wa Spika wa Bunge Job Ndugai.

Wekundu hao wa Msimbazi wamewasili jijini hapo leo alfajiri na kesho watacheza mechi ya kiporo dhidi ya Dodoma Jiji FC saa 10 jioni kabla hawajarudi Dar kuikabili Azam FC Jumapili Februari 7.

Simba wiki iliyopita walishinda kombe la Super Cup waliloshinda katika mashindano waliyoyaandaa wiki iliyopita yalisorokisha timu za Al Hilal ya Sudan na TP Mazembe ya Congo.