Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba SC yamtambulisha Abdulrazack kutoka Super Sport

Muktasari:

  • Simba imemtambulisha mchezaji huyo mchana huu, ikiwa ni muendelezo wa hatua ya kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na Michuano ya Kimataifa.

Klabu ya Simba imemsajili Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba imemtambulisha mchezaji huyo mchana huu, ikiwa ni muendelezo wa hatua ya kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na Michuano ya Kimataifa.

Taarifa ya Simba iliyochapishwa kwenye mitandao yake ya kijamii inasema kuwa Abdulrazack ana umri wa miaka 21, bado ana nguvu na muda mrefu wa kucheza soka.

“Abdulrazack ana umri wa miaka 21 bado ana nguvu na muda mrefu wa kucheza soka na tunaamini atakuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi chetu.

“Abdulrazack ni mchezaji kijana wa Kitanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini kwa ubora mkubwa akiwa kwenye kikosi cha kwanza.

“Ukiacha ubora alionao na umri wake ni mchezaji ambaye anaijua vizuri Ligi ya Tanzania kwa kuwa amecheza kwa ubora katika timu za Mbeya City, KMC na Namungo FC,” imeeleza taarifa hiyo ya Simba