Simba, Lipuli zapishana, Bongo Zozo aamsha shangwe

Muktasari:
Kwa upande wa mashabiki, wameanza kuingia uwanjani hapo tangu saa 5:00 asubuhi, lakini mtaani hakukuwa na amsha amsha zozote za mashabiki kama ilivyozoeleka kwa timu za Lipuli, Simba au Yanga zinapokuwa na mechi mjini Iringa amsha amsha za mashabiki huanza asubuhi kwa kupita mitaani wakitoa burudani za tofauti tofauti.
SIMBA na Lipuli FC zimepishana dakika tano kuingia Uwanja wa Samora mjini Iringa kwa ajili ya mechi yao inayotarajia kuanza muda mchache kuanzia sasa huku shabiki wa soka nchini, Bongo Zozo akiwa kivutia uwanjani hapa.
Simba ndiyo wamekuwa wa kwanza kuingia uwanjani wakitumia basi lao na wameingia saa 8:47 wakati wenyeji wao Lipuli wameingia saa 8:52 nao wakitumia basi lao aina ya Coaster.
Kwa upande wa mashabiki, wameanza kuingia uwanjani hapo tangu saa 5:00 asubuhi, lakini mtaani hakukuwa na amsha amsha zozote za mashabiki kama ilivyozoeleka kwa timu za Lipuli, Simba au Yanga zinapokuwa na mechi mjini Iringa amsha amsha za mashabiki huanza asubuhi kwa kupita mitaani wakitoa burudani za tofauti tofauti.
Hata, hivyo shabiki wa Taifa Stars, Bongo Zozo amekuwa kivutio kwa mashabiki baada ya kuingia kwa kutumia gari la wazi aina ya Noah Vox huku akiwa amevalia jezi ya Lipuli.
Bongo Zozo baada ya kushuka ameonekana mwenye furaha na kwenda kwa mashabiki jukwaani na kusalimiana nao huku akishangiliwa.
Bongo Zozo ametangaza kuwa yeye ni shabiki wa Lipuli Fc.