Simba kukiwasha na na Saint George Simba Day

Thursday August 04 2022
simba day pic
By Imani Makongoro

Klabu ya Simba imethibitisha kucheza na St George katika kilele cha Siku ya Simba 'Simba Day' Agosti 8.

Nyota wa klabu hiyo kongwe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ethiopia watawasili nchini Agosti 6 tayari kwa mechi hiyo ya kimataifa wa kirafiki.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema timu hiyo itawasili ikiwa na nyota wake wote tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

"Wapinzani wetu watawasili Dar es Salaam siku mbili kabla ya kilele cha Simba day Agosti 8," amesema.

Simba inafanya tamasha hilo kwa mara ya 14 msimu huu tangu lilipoanzishwa mwaka 2009, pamoja na shamra shamra nyingine, watalitumia kutambulisha wachezaji wao wapya kabla ya kucheza mechi hiyo ya kimataifa ya kirafiki.

Advertisement