Simba kuamua hatima ya Ruvu shooting kubaki Ligi Kuu Bara

Muktasari:
- Simba ipo nafasi ya pili na pointi 64 huku Ruvu Shooting ikishika mkia na pointi 20.
Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni roundi 28 na leo Simba inawakaribisha Ruvu Shooting katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Ruvu Shooting huu ni mchezo unaoamua hatima yao ya kusalia Ligi Kuu na itashuka rasmi daraja ikiwa itafungwa na Simba na endapo KMC ikashinda au kutoka sare na Singida Big Stars.
Simba ipo nafasi ya pili na pointi 64 huku Ruvu Shooting ikishika mkia na pointi 20.