Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Fountain Princess kumalizana Dodoma

Simba, Fountain Princess kumalizana Dodoma

Muktasari:

  • Mchezo wa mwisho baina ya timu hizo, Fountain Gate Princess waliibuka na ushindi wa bao 1-0 uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Dodoma. BAADA ya kumalizana kwenye ubingwa wa Ligi Kuu wanawake msimu uliopita ambao Simba Queens walifanikiwa kuendeleza ubabe, timu za Fountain Gate na Simba Queens zitakuwa na kibarua cha mwisho kumaliza ubishi baina yao.
Ubishi huo utamalizwa kwenye mashindano maalum ya Gets International yanayotarajiwa kuchezwa kuanzia Julai 15 hadi 24 jijini Dodoma, ambapo timu nane zitashiriki kusaka mbabe wa soka la wanawake pekee.
Ni katika mashindano hayo ndipo timu hizo mbili zitakutana kwa mara nyingine, baada ya kukutana hivi karibuni kwenye ule mchezo maalum ulioshuhudia Fountain Gate Princess wakibeba taji mbele ya Simba Queens kupitia bao la Rehema Ramadhani.
Ili kukutana kwenye mchezo wa fainali kuwania kombe, timu hizo zitapaswa kufanya kazi ya ziada kuzishinda timu pinzani ikiwemo nne kutoka nje ya nchi ambazo zimealikwa na kuthibitisha kushiriki.
Timu hizo ni Ulinzi Starlets, Kenyata University na SGF Barcelona zote za Kenya na CFC Amani ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, pamoja na timu mbili nyingine za ndani ambazo ni Gets FC na Alliance Girls.
Mratibu wa mashindano hayo, Kelvin Herry amethibitisha timu zote kuanzia Simba Queens na zile nne za nje kuthibitisha kushiriki mashindano hayo yatakayofanyika majira ya jioni na usiku kwenye uwanja wa Fountain Gate Arena unaowekwa taa.
''Timu zote zimethibitisha kushiriki ikiwemo wapinzani wakubwa kwa soka la wanawake nchini, Simba Queens na Fountain Princess pamoja na zile za Kenya na Congo, kwa mara ya kwanza mechi hizo zitachezwa usiku kutokana na kukamilika kwa uwekwaji taa ndani ya uwanja wa FGA Arena''. alisema Herry.
Simba Queens imeelezwa kushiriki mashindano hayo ili kujiweka sawa kabla ya kwenda kushiriki mashindano ya mabingwa wa ukanda wa Afrika Mashariki (Cecafa) yatakayofanyika jijini Arusha mwaka huu.