Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Silaha za Man City zipo tayari kuivaa Liverpool

Muktasari:

  • Kikosi cha Pep Guardiola kinahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji Ligi Kuu England.

England. Timu ya Manchester City imenoa silaha zake jana Jumatatu jioni katika mazoezi yake kabla ya kuikabili Liverpool kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya unaotarajiwa kupigwa kesho Jumatano usiku.
Kikosi cha Pep Guardiola kinahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji Ligi Kuu England.
Barani Ulaya macho ya mashabiki wa soka macho yote yataigeukia mechi hiyo ili kuipa nafasi timu itakayoibuka na ushindi kutinga nusu fainali ya msahindano hayo.
Man City inaingia kifua mbele katika mechi hiyo kesho ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wake wa mwishoni mwa wiki baada ya kuifunga Everton kwa mabao 3-1.
Timu hiyo ya Etihad itashuka uwanjani akili yake ikiwa imeelekeza kwa nyota Kevin De Bruyne na Sergio Aguero wakisaidiana na Raheem Sterling, Bernardo Silva na Gabriel Jesus.