Shabiki wa Simba SC ashinda Sh125 milioni aahidi kufungua tawi la Simba Mbozi

Muktasari:
Ninafuraha baada ya kushinda pesa hii, lakini mbali ya matumizi ambayo nitakwenda kuwekeza na pesa iweze kujizalisha sitaacha kuanzisha tawi la Simba pale kwetu Mbozi
Dar es Salaam.Shabiki wa Simba SC, Mussa Mwangoka kutokea Mbeya ameshinda Sh125 milioni baada ya kubeti mechi 12, kupitia kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Premier Bet, na leo Alhamisi alikabidhiwa kiasi chake.
Mwangoka alisema alibeti mechi 12, kupitia Premier Bet, ambazo alizipatia zote na kushinda pesa hiyo ambayo katika tangu kuzaliwa kwake hajawahi kuishika na kazi ambayo atakwenda kuifanyia ni kuanzisha biashara, lakini hatasahau kufungua tawi la Simba wilaya ya Mbozi huko Mbeya.
"Ninafuraha baada ya kushinda pesa hii, lakini mbali ya matumizi ambayo nitakwenda kuwekeza na pesa iweze kujizalisha sitaacha kuanzisha tawi la Simba pale kwetu Mbozi kwani ni timu ambayo naipenda na huwa naifuata katika mikoa mbalimbali kuishangilia," alisema.
"Nimepata wakati mgumu kutafuta pesa za kwenda kuiangalia timu yangu ya Simba, lakini pesa hii ambayo nimeshinda kupitia Premier Bet, itakwenda kurahisisha hilo, lakini niwaambie marafiki zangu na wadau wa kucheza michezo hii hili ni jambo la kweli na haki," alisema Mwangoka.
Meneja masoko wa Premier Bet, Benjamini Mnari alisema kampuni yao inashauri wateja wake kuwa michezo ya kubahatisha si ajira au chanzo cha kupata kipato bali ni burudani ndio maana washindi wengi wamekuwa wakipatikana mara kwa mara.
"Tumpongeze mshindi wetu Mwangoka kwani si kazi rahisi kubeti mechi 12, na zote zikatoka kama ambavyo iliweka lakini niwakaribishe wadau na wapenzi wa soka wa timu mbalimbali hapa nchini kama Simba, Yanga, Azam na nyinginezo kuanzia miaka 18, kucheza michezo hii ya kubahatisha kupitia kampuni ya Premier Bet kwani kushinda kwetu ni rahisi," alisema Mnari.