Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beno Ngassa ajibana Dodoma Jiji

NGASSA Pict

Muktasari:

  • Ngassa alikuwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha Tanzania Prisons kilichokuwa kinanolewa na kocha Aman Josiah ambapo tangu kocha huyo atue hapo Januari, mwaka huu, amefunga mabao matano na asisti tatu.

WINGA machachari, Beno Ngassa amejiunga na timu ya Dodoma Jiji kwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia katika msimu ujao.

Ngassa alikuwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha Tanzania Prisons kilichokuwa kinanolewa na kocha Aman Josiah ambapo tangu kocha huyo atue hapo Januari, mwaka huu, amefunga mabao matano na asisti tatu.

Mwanaspoti linafahamu nyota huyo alikuwa anafuatiliwa kwa muda mrefu na suala ambalo lilikuwa limebaki ni kuona namna ambavyo anamaliza Ligi.

Chanzo kutoka ndani ya Dodoma Jiji kililidokeza gazeti hili kwamba nyota huyo ni pendekezo la benchi la ufundi tangu Ligi ilipokuwa inaendelea.

“Lilikuwa ni suala la muda juu ya kusajiliwa kwa sababu benchi la ufundi na Uongozi kiujumla walikuwa na mipango ya kumsajili,” kilisema chanzo hicho.

Usajili huo unaenda kuongeza nguvu kwenye eneo la winga katika kikosi cha Dodoma baada ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili mchezaji wao Idd Kipagwile.

Uongozi wa Dodoma bado unaendelea kusuka kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu baada ya msimu uliomalizika 2024/25 kumaliza nafasi ya 12 kati ya timu 16 ikikusanya pointi 34.