Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yasisitiza Uwanja wa Mkapa uko tayari kwa Dabi ya Kariakoo Juni 15

DABI Pict

Muktasari:

  • Itakumbukwa kuwa, awali pambano hilo la watani lilikuwa lipigwe Machi 8, mwaka huu kabla ya kuahirishwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), baadae kulipangia kuchezwa Juni 15, mwaka huu.

SERIKALI imethibitisha kuwa, Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam uko tayari kwa kuchezwa pambano kubwa la watani wa jadi hapa nchini, Yanga dhidi ya Simba litakalopigwa Juni 15, 2025.

Katika kipindi cha Maswali na Majibu mapema leo, Ijumaa Mei 30, 2025, bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA', alijibu swali la Naibu Spika, Mussa Hassan Zungu, kuhusu hatma ya mechi hiyo kufuatia ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Zungu alitaka kufahamu iwapo Uwanja wa Mkapa utakuwa tayari kwa mechi hiyo, huku akitumia kauli ya utani kuuliza: “Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri, tarehe 15, Mnyama (Simba) yupo kwa Mkapa?”

Mwana FA amethibitisha pasi na shaka kuwa: “Tarehe 15 Mnyama yupo kwa Mkapa, wakipambana na mahasimu wao Yanga.”

Itakumbukwa kuwa, awali pambano hilo la watani lilikuwa lipigwe Machi 8, mwaka huu kabla ya kuahirishwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), baadae kulipangia kuchezwa Juni 15, mwaka huu.

Hata hivyo, pamoja na kuwapo kwa ratiba ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara duru la pili, baadhi ya viongozi wa Yanga wameendelea kusisitiza kuwa hawako tayari kucheza mchezo huo, wakishinikiza kupewa majibu ya kilichosababisha tarehe ya kwanza mchezo kuahirishwa.