Serengeti wapania makubwa Afcon mwakani

Dar es Salaam. Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo amesema kupitia mashindano yaliomalizika jana Jumapili jijini Dar es Salaam, anaamini yamewapa hatua na uzoefu kuelekea fainali za AFCON zitakazofanyika mwakani nchini.
Milambo anasema alichokuwa anakiangalia katika michuano hiyo ni ubora na mapungufu kwa vijana wake, lengo ni kukisuka mapema ili mwakani kiweze kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
"Lengo letu ni kuhakikisha tunacheza AFCON na Kombe la Dunia, vijana wanapambana kwa sasa nimewapa mapumziko ya wiki mbili kisha watarejea kambini kuendelea na mandalizi ya michuano hiyo ya mwakani.
"Hatuna haja ya kuchagua kambi itakuwa wapi wakati michuano hiyo itafanyika Tanzania, kikubwa ni wadau waendelee kuwaunga mkono vijana wao ambao wanaonyesha wa nia ya kutaka kulifanyia kitu taifa lao,"alisema Milambo.