Serengeti Boys yajisafisha makosa ya Uturuki

Muktasari:
Aliwataka wachezaji wake kupiga krosi ndefu na fupi kwa ufasaha na zoezi hilo lilipokuwa linakosewa walikuwa wanarudia mpaa wapatie.
BAADA ya kukamilisha katika zoezi la kushambukia kwa spidi, kocha Oscar Milambo wa Serengeti Boys amehamia katika zoezi la kucheza mipira ya faulo.
Katika mazoezi yanayoendelea kwenye Uwanja wa Jk Youthpark, Milambo aliwapa zoezi maalum wachezaji wake kuwa wepesi katika kupiga krosi lakini vilevile kwenye uokoaji.
Aliwataka wachezaji wake kupiga krosi ndefu na fupi kwa ufasaha na zoezi hilo lilipokuwa linakosewa walikuwa wanarudia mpaa wapatie.
Kwa upande wa mabeki waliokuwa wanacheza faulo hizo, walikuwa wanatakiwa kuokoa mashambulizi kwa uharaka ili adui asipate muda wa kucheza mpira langoni mwao.
Makipa nao walikuwa na kazi muhimu ambapo mda wote Manyika Peter alikuwa yupo makini katika kuwaelekeza kucheza mipira ya krosi.
Baada ya zoezi hilo Milambo aliwapa wachezaji wake zoezi la kurusha mipira (Throw In) lakini aliwataka wasirushe mipira kwa nyuma badala yake warushe kwa spidi kuelekea kwa wapinzani wake na aliwataka washambuliaji wake Kelvin John na Maurice Abraham wasiwe na mambo mengi wanapokuwa golini.