Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys wanamikwara hao!

Dar es Salaam. Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania ‘Serengeti Boys’, Oscar Milambo, amefichua kuwa anayatumia mashindano ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wa umri huo Afcon 2019, kuwatengeneza vijana wake kisaikolojia.

Alisema kuwa suala la saikolojia ni muhimu kwa vijana wake na kuwa amekuwa akimfuatilia mchezaji mmoja baada ya mwingine na mwisho wa siku anaketi nao ili kuondoa udhaifu aliouona kwa kila mmoja.

Milambo alisema kuwa wanayatumia mashindano hayo kuyaondoa makosa ya mchezo unaotangulia akiamini mpaka yatakapofika tamati kikosi kitakuwa kimeiva.

Alisema ingawa Serengeti Boys imeshafuzu kwa fainali hizo za mwakani lakini hawabweteki kwa kuwa nia yao ni kuhakikisha wanafanya vizuri nia ikiwa kutwaa ubingwa huo wa Afrika kwa vijana.

“Mechi hizi sisi hatuzichukulii wepesi tumekuwa tukiwahamasisha vijana wetu wachukulie kama mechi zingine za mashindano,” alisema na kuongeza.

Alisema kuwa anafuraha kuona vijana wake wanatekekeleza kile anachowaelekeza ikiwa ni ishara kuwa watatoa matokeo mwakani.

Kikosi cha Serengeti Boys kinatarajiwa kushuka dimbani leo katika mchezo wa pili kucheza na Sudan, katika mchezo wa kwanza ilibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Burundi.