Serengeti Boy kukinukisha leo tena

Muktasari:
- Tanzania na Rwanda zote zimeshafuzu kutoka Kundi A, lakini mechi ya leo ni ya kujenga heshima na kusaka mshindi wa kwanza n wa pili ili kujua wa kucheza naye katika mechi za nusu fainali dhidi ya washindi wa Kundi B.
Dar es Salaam. HAINA cha kupoteza kwani tayari imeshakata tiketi ya nusu fainali. lakini timu ya taifa ya Vijana U17, Serengeti Boys imesisitiza leo Alhamisi wataendeleza tena moto wao kwa Rwanda katika mechi ya kuwania Afcon 2019 kwa Kanda ya Cecafa.
Tanzania na Rwanda zote zimeshafuzu kutoka Kundi A, lakini mechi ya leo ni ya kujenga heshima na kusaka mshindi wa kwanza n wa pili ili kujua wa kucheza naye katika mechi za nusu fainali dhidi ya washindi wa Kundi B.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Oscar Milambo, alisema hawatabweteka kwa vile wamefuzu nusu fainali, badala yake amedai anahitaji kuweka heshima kwa kila mechi watakayocheza vijana wake.
Milambo alisema vijana wake wapo imara kuhakikisha wanaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuweka heshima ya kuwafunga Rwanda, aliodai ina ushindani wa hali ya juu.
"Tunatarajia sapoti ya mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani, ili kuwaunga mkono vijana wao ambao wanafarijika kuona umati mkubwa unapokuwa umefika uwanjani, niwaambie licha ya kutokuwa na chakupoteza badohatubweteki."
Naye nahodha wa Serengeti Boys, Morice Abraham alisema wataendelea kufanya mazuri kuuthuibitishia umma kwamba wao ni wawakilishi wazuri na kuwaomba wafurike Uwanja wa Taifa kuwaunga mkono.
Kwa upande wa kocha wa Rwanda, Rwasamanzi Yves alisema licha ya kuiheshimu Serengeti lakini bado amebaini mapungufu anayoweza kuyatumia kuwanyanyasa katika mechi ya leo.
Tanzania na Rwanda zinasuiri kujua zitacheza na nani kutoka Kundi B ambalo timu za Kenya, Uganda na Ethiopia zipo kwenye vita ya kuwania nafasi mbili za kusonga mbele. Djibouti na Sudani Kusini zilishaaga mapema katika kundi hilo.