Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saliboko mikononi mwa maafande

SALIBOKO Pict

Muktasari:

  • Mmoja wa watu wa karibu na mchezaji huyo, aliliambia Mwanaspoti Saliboko ameanza mazungumzo na mabosi wa JKT, licha ya KMC pia kumuwekea mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho cha Kinondoni jijini Dar es Salaam.

MAAFANDE wa JKT Tanzania wako katika mazungumzo kwa ajili ya kuipata saini ya mshambuliaji wa KMC FC, Daruweshi Saliboko ili kuichezea timu hiyo msimu ujao, baada ya kuonyesha nia ya kuhitaji kuondoka kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya.

Mmoja wa watu wa karibu na mchezaji huyo, aliliambia Mwanaspoti Saliboko ameanza mazungumzo na mabosi wa JKT, licha ya KMC pia kumuwekea mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho cha Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“JKT imeonyesha nia ya kumuhitaji na tayari mazungumzo yanaendelea licha ya ushindani mkubwa uliopo kutoka pia kwa timu nyingine zinazomuhitaji, naamini siku zijazo mbele tutafikia sehemu nzuri ya makubaliano rasmi,” kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungula, alisema mikakati ya kuwaongezea mikataba nyota waliomaliza inaendelea, kwani wao kama viongozi wanaendelea kupitia ripoti ya benchi la ufundi na kuifanyia kazi kwa uharaka zaidi.

“Ripoti ya benchi la ufundi ndio itakayotupa mwanga wa kutambua ni wachezaji gani wa kuwaongezea mikataba kwa wale ambao wamemaliza au kuachana nao na kuangalia wengine wapya, tutafahamu hilo kwa siku zijazo mbele,” alisema Mwakasungula.

Nyota huyo aliyezichezea timu za, Lipuli FC na Polisi Tanzania, msimu huu wa 2024-2025 amefunga mabao mawili ya Ligi Kuu Bara, aliyofunga yote dhidi ya Tanzania Prisons, kwenye ushindi wa KMC wa mabao 2-1, mechi iliyopigwa, Oktoba 26, 2024.