Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salamba aanza kukumbuka vyakula vya Tanzania, wali wa Kuwait hausomeki

Muktasari:

Salamba alisema kama kuna kitu anapata nacho shida ni vyakula vyao ambavyo havielewi, tofauti na vya Tanzania na kukiri vinampa wakati mgumu.

Dar es Salaam. Mshambuliaji Adam Salamba ameanza kukumbuka wali na vyakula vya Tanzania akidai anapata wakati mgumu kuzoea chakula na lugha huko Kuwait anakocheza soka la kulipwa katika timu ya Al Jahra SC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza  ‘Kuwait Division One’.
Salamba alisema kama kuna kitu anapata nacho shida ni vyakula vyao ambavyo havielewi, tofauti na vya Tanzania na kukiri vinampa wakati mgumu.
Salamba alitaja changamoto nyingine nje na chakula ni anapata wakati mgumu kuwasiliana na wenyeji wake ambao wanazungumza Kiarabu.
“Vyakula vya huku ni tofauti na Tanzania, wali wao hauna ladha angalau viazi vya chipsi ndio havina utofauti na huko kwetu, kuhusu lugha kuna Wacameroon ambao wamekaa kwa muda mrefu huku angalau wanajua Kiarabu.”
“Kuhusu mazingira hayanisumbui sana, shida Kiarabu kwa sababu kuna wakati mwingine nataka kuwasaliana na viongozi moja kwa moja nashindwa, lazima nipitie kwa Wacameroon.”
“Kuhusu soka la huku lina ushindani ingawa nimecheza mechi ya kirafiki, nikaumia nyama ya paja, lakini naona watu wanavyopambana uwanjani, natakiwa kujituma ili kufikia malengo yangu”alisema.