Saido aitwa fasta Yanga

Saido aitwa fasta Yanga

Muktasari:

STAA mpya wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza atakanyaga kwenye ardhi ya Dar es Salaam kesho saa 3:40 usiku tayari kuanza kazi Jangwani.

STAA mpya wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza atakanyaga kwenye ardhi ya Dar es Salaam kesho saa 3:40 usiku tayari kuanza kazi Jangwani.

Mwanaspoti linajua Kocha Cedrick Kaze ameagiza mchezaji huyo aje haraka kabla ya dirisha kufunguliwa ili ajue nini cha kufanya.

Habari zinasema kwamba Kocha anafikiria kusajili straika mwingine lakini ni kama hataridhishwa na ubora wa Saidi.

“Kocha ametaka aje kwa haraka ili kuangalia anaingiaje kwenye mfumo wake, lakini kama akifanya kile kinachotakiwa hatasajili straika mwingine ataleta beki na kiungo,” alidokeza mmoja wa vigogo wa usajili wa Yanga.

Habari zinasema kwamba Kaze atakaa na viongozi wa Yanga wiki hii kufanya uamuzi kuhusiana na mabadiliko ya kwenye dirisha dogo lakini bado imekuwa ni siri kubwa ndani.


KAZE ANACHOTAKA

“Eneo jingine ambalo nimefanikiwa ni kutengeneza safu ya kiungo imara ambayo ina uwezo wa kufanya kazi mbili kuzuia mashambulizi ya timu pinzani na kuanzisha mashambulizi ambayo ndani yake hutengeneza nafasi nyingi za kufunga na muda mwingine kufunga wenyewe,” alisema.

“Mastraika wangu pengine kama wangekuwa watulivu na kutumia nafasi hizo za kufunga kama ninavyowaelekeza katika mazoezi na mbinu ambazo nawapatia pengine tungekuwa tumefunga zaidi ya mabao 15,” alisema Kaze.

Katika kikosi cha Yanga, mastraika Michael Surpong amefunga mabao matatu, Yacouba Sogne, Wazir Junior kila mmoja amefunga bao moja na Ditram Nchimbi ambaye muda mwingine anacheza kama winga hajafunga bao lolote.

“Nitakaa na viongozi wangu kabla ya dirisha kufunguliwa na kuwajadili mwenendo wa mastraika ambao tunao sasa ili kuona wanatufaa au kununua mwingine ambaye atakuwa na sifa ambazo tuliokuwa nao wakati huu hawana,” alisema Kaze.