Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rupia atupia mbili akimng'oa Gomez kileleni

Rupia Pict
Rupia Pict

Muktasari:

  • Mabao hayo mawili yaliyopatika kwenye Uwanja wa Liti, mjini Singida yamemfanya Rupia kufikia mabao saba, ikiwa ni moja zaidi na aliyokuwa nayo Gomez aliyekaa kileleni mwa orodha ya wafungaji kwa muda mrefu, japo nyota huyo wa Fountain kesho anatarajiwa kushuka uwanjani kukabiliana na Coastal Union.

STRAIKA nyota wa Singida Black Stars, Elvis Rupia mchana huu ametupia mbaoa mawili wakati timu hiyo ikiinyoa Dodoma Jiji 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara na kumfanya akae kileleni mwa orodha ya wafungaji wa ligi hiyo akimuengua Seleman Mwalimu 'Gomez' wa Fountain Gate.

Mabao hayo mawili yaliyopatika kwenye Uwanja wa Liti, mjini Singida yamemfanya Rupia kufikia mabao saba, ikiwa ni moja zaidi na aliyokuwa nayo Gomez aliyekaa kileleni mwa orodha ya wafungaji kwa muda mrefu, japo nyota huyo wa Fountain kesho anatarajiwa kushuka uwanjani kukabiliana na Coastal Union.

Katika mchezo huo wa leo, Rupia alifunga bao la kwanza dakika ya nane akimalizia pasi tamu ya beki Tra Bi Tra kabla ya kuongeza lingine dakika ya 15 kwa kichwa akipokea pasi murua kutoka kwa kiungo Josephat Bada na kuipeleka Singida mapumziko ikiwa mbele kwa 2-0.

Kipindi cha pili Dodoma Jiji inayonolewa na kocha Mecky Maxime ilifanya mabadiliko kadhaa na kuongeza kazi ya kulishambulia lango la wenyeji na katika dakika ya 58 juhudi zao zilizaa matunda kwa Yassin Mgaza kumalizia kwa kichwa, pasi murua kutoka kwa mshambuliaji, Paul Peter.

Matokeo hayo yameziacha timu zote mbili katika nafasi zilizokuwapo awali Simba ikiwa ya nne ikifikisha pointi 27 kama ilizonazo Yanga ikicheza mechi 13, sawa na zile ilizocheza Dodoma Jiji iliyoshika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 16.

Mechi nyingine ya ligi hiyo inaendelea jioni kwa pambano kati ya KMC na Mashujaa zinazovaana kwenye Uwanja wa KMC, uliopo Mwenge Jiji Dar es Salaam.