Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prisons, Mbeya City kitaumana Sokoine ';Playoff'

Muktasari:

  • Kocha Mkuu wa Mbeya City, Salum Mayanga alisema hakuna namna nyingine zaidi ya kwenda kujipanga na vijana wake kuhakikisha wanashinda mechi zote na kubaki salama.

WAKATI wadau na mashabiki wa soka jijini Mbeya wakitamba kuwa na uhakika wa timu moja Ligi Kuu msimu ujao, makocha wa Tanzania Prisons na Mbeya City wameanza kuchora ramani ya kutoboa katika mechi za mchujo (play off) itakayochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Prisons na Mbeya City zinatarajia kukutana Julai 5 katika mchezo wa mkondo wa kwanza kupambania kubaki Ligi Kuu msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya 13 na 14.

Mbeya City iliyomaliza na pointi 30 ndio watakuwa wenyeji wa mchezo huo kabla ya kurudiana siku tatu baadaye na mshindi wa jumla atajihakikishia kubaki Ligi Kuu, huku mpinzani akisubiri mshindi wa Championship baina ya Polisi Tanzania na Mbeya Kwanza.

Hata hivyo, timu hizo za jijini Mbeya ni mara ya pili kucheza play kwa misimu tofauti, ambapo Tanzania Prisons iliwahi kucheza mchujo huo ilipokutana na JKT Tanzania na kushinda jumla ya mabao 2-1.

Mbeya City wao wanarejea kwenye mtihani huo wakiwa na kumbukumbu mbaya walipoondolewa na Mashujaa FC kwa jumla ya mabao 3-2, huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa ndugu hao kukutana kwenye play off.

Kama haitoshi, ndugu hao wanatarajia kukutana kwa mara ya nne msimu huu ambapo mechi za kawaida Ligi Kuu walikutana mara mbili huku kila mmoja akishinda mchezo mmoja na sasa wanaenda kukutana tena kusaka heshima upya.

Kocha Mkuu wa Mbeya City, Salum Mayanga alisema hakuna namna nyingine zaidi ya kwenda kujipanga na vijana wake kuhakikisha wanashinda mechi zote na kubaki salama.

“Kwenye mpira lazima uwe tayari kupokea chochote kinachotokea, tumejaribu kupambana, lakini hatujaweza, kikubwa ni kujipanga na wenzetu Prisons, tutajiandaa kushinda,”€  alisema Mayanga.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Shedrack Nsajigwa amesema baada ya kufanikiwa kukwepa kushuka daraja moja kwa moja ni mafanikio ya kwanza na sasa dakika 180 zilizobaki ni jasho na damu kufanya kweli. “Tunashukuru vijana wamepambana kadri walivyoweza hadi kukwepa aibu ya kushuka moja kwa moja, nguvu hii, nia na juhudi tulizoonesha tunazielekeza zaidi kwa mechi za mchujo tubaki salama,”€  alisema Nsajigwa.