Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo, Neymar walivyochangia timu zao pesa ndefu za usajili

Muktasari:

Kwa mujibu wa Transfermarkt, hizi hapa ndizo klabu 10 zilizopiga pesa ndefu kwa kuuza wachezaji ndani ya miaka 10 iliyopita kuanzia msimu wa 2009/10.

LONDON,ENGLAND. HAKUNA klabu inayotaka kuuza wachezaji wao bora. Lakini, wakati mwingine inakuwa haina ujanja, lazima litokee hilo.

Kama mchezaji husika anataka kuondoka, au kuna klabu imeleta ofa tamu ambayo ni ngumu kuigomea, klabu zimekuwa haziweki ngumu kwenye kufungulia milango wachezaji ili kuingiza mkwanja.

Kwa mujibu wa Transfermarkt, hizi hapa ndizo klabu 10 zilizopiga pesa ndefu kwa kuuza wachezaji ndani ya miaka 10 iliyopita kuanzia msimu wa 2009/10.

10.Liverpool - Pauni 691.47milioni

Liverpool wameingia kwenye orodha hii ya timu zilizopiga pesa nyingi kupitia wachezaji wake ndani ya miaka 10 iliyopita. Ndani ya muda huo, Liverpool imewapiga bei Philippe Coutinho na Luis Suarez walipokwenda Barcelona kwa pesa nyingi, wakati Fernando Torres alipigwa bei kwenda Chelsea kwa ada ya Pauni 50 milioni. Ndani ya muda huo, Liverpool waliweka kibindoni mkwanja unaozidi Pauni 600 milioni kwa kuuza mastaa wake licha ya kuwahi kuingia mkenge kwa kuwasajili Mamadou Sakho, Christian Benteke na Jordan Ibe.

9.Porto - Pauni 717.03milioni

FC Porto wameonekana kuwa na kawaida ya kupiga bei moja ya wachezaji wake bora katika kila msimu. Msimu huu walimruhusu staa wao Eder Militao kwenda kujiunga Real Madrid kwa ada ya Pauni 45 milioni. Huko nyuma, ilifungua milango ya kuwaruhusu mastaa wake matata kama Radamel Falcao, Jackson Martinez na Lisandro Lopez. Hata hivyo, jambo hilo limewaingizia pesa nyingi sana na kuifanya FC Porto kuwa moja ya timu zilizopiga pesa nyingi kwa kuuza wachezaji wake ndani ya miaka 10 iliyopita.

8.Real Madrid - Pauni 731.21milioni

Ni moja ya timu zilizotumia pesa nyingi kwenye usajili, lakini Real Madrid ni miongoni pia kwa klabu zilizopiga mkwanja mrefu kwa kupiga bei mastaa wake. Kuuzwa kwa staa kama Cristiano Ronaldo kwenda Juventus kumeingizia pesa nyingi timu hiyo, sambamba na Angel Di Maria alipopigwa bei kwenda Manchester United. Ndani ya muda huo wa miaka 10 iliyopita, Los Blancos wamepiga pesa ndefu zaidi ya Pauni 700 milioni kupitia mauzo ya wachezaji wake.

7.AS Roma - Pauni 745.34milioni

Liverpool ndio waliowafanya AS Roma kupiga pesa ndefu zaidi wakati ilipowasajili Mohamed Salah na Alisson Becker kwa zaidi ya Pauni 100 milioni. Kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, Giallorossi walipiga bei mastaa wake kadhaa akiwamo Kostas Manolas, Stephan El Shaarawy na Luca Pellegrini ambao waliichangia timu hiyo pesa ndefu na kuifanya iingize zaidi ya Pauni 700 milioni katika kupiga bei mastaa wake muhimu kwenye kikosi.

6.Barcelona - Pauni 748.89 milioni

Supastaa Neymar alipoondoka Barcelona kwenda Paris Saint-Germain jambo hilo liliwaingizia wakali hao wa Nou Camp mkwanja unaokaribia Pauni 200 milioni. Ndani ya miaka 10 iliyopita, Barcelona wamepiga pesa ndefu zaidi ya Pauni 700 milioni kwa kuuza mastaa wake, ambapo miongoni mwao ni Cesc Fabregas na Alexis Sanchez waliopigwa bei kwa pesa nyingi wakiichangia timu zaidi ya Pauni 60 milioni. Wachezaji wengine walioondoka Nou Camp kwa pesa nzuri ni Jasper Cillessen, Yerry Mina, Paulinho na Malcom.

5. Juventus -Pauni 806.72milioni

Juventus ilimpiga bei Paul Pogba kwa ada iliyoweka rekodi ya dunia Pauni 89 milioni mwaka 2016. Ulikuwa mkwanja mrefu ambao uliwafanya Liverpool kuingia kwenye orodha ya timu zilizoingiza pesa nyingi kwa kuuza mastaa wake. Wachezaji wengine ambao waliachana na miamba hiyo ya Serie A kwa pesa nyingi na kuingizia klabu faida ni Joao Cancelo, Leonardo Bonucci na Arturo Vidal. Kwenye kikosi cha Juventus kwa sasa kuna mastaa kibao kama Cristiano Ronaldo na bila ya shaka wengine watauzwa kupiga pesa.

4.Chelsea - Pauni 820.24milioni

Chelsea imepoteza wachezaji wake muhimu kwa miaka ya karibuni baada ya Eden Hazard na Diego Costa wote kuondoka kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge kwa dili za pesa nyingi. Lakini, The Blues ilipiga pesa ndefu pia kwa kuwauza mastaa kama Oscar, Alvaro Morata, David Luiz, Juan Mata, Nemanja Matic, Romelu Lukaku, Thibaut Courtois na Arjen Robben, ambao waliondoka kwa zaidi ya Pauni 30 milioni kila mmoja na kufanya wakali hao wapige mkwanja unaozidi Pauni 800 milioni kwenye biashara ya wachezaji.

3.Atletico Madrid - Pauni 878.4milioni

Atletico Madrid uwezo wao wa kutengeneza mastraika wa kiwango cha dunia kimewafanya kupiga mkwanja mrefu ndani ya miak 10 kutokana na kuwauza mastaa hao. Miamba hiyo ya Hispania, imeweka kibindoni zaidi ya Pauni 800 milioni kwa kuuza wachezaji wake ndani ya muda huo, huku mastraika wa maan waliopigwa bei na wakali hao wa Wanda Metropolitano ni Antoine Griezmann, Radamel Falcao, Jackson Martinez, Sergio Aguero, Diego Costa na Fernando Torres ambao wote wameingizia timu pesa ndefu.

2.Monaco - Pauni 894.1milioni

Ni jambo la wazi, Kylian Mbappe ndiye mchezaji aliyeiingizia AS Monaco pesa nyingi zaidi wakati walipompiga bei kwenye Paris Saint-Germain. Straika huyo Mfaransa aliuzwa kwa Pauni 165 milioni huku Monaco ikipiga mkwanja mrefu, zaidi ya Pauni 800 milioni kwenye kuuza wachezaji ndani ya miaka 10 iliyopita. Wachezaji wengine wa Monaco waliouzwa kwa pesa nyingi ni James Rodriquez, Thomas Lemar na Anthony Martial, ambao wamepigwa bei kwa zaidi ya Pauni 50 milioni kwa kila mmoja.

1.Benfica - Pauni 909.9milioni

Benfica wapo vizuri kwenye kupiga pesa kwa kuuza mastaa wake, ambapo ndani ya miaka 10 wababe hao wa Ureno wamevuna zaidi ya Pauni 900 milioni. Ndani ya muda huo, Benfica imepiga bei mastaa kama Joao Felix kwa Pauni 113 milioni, Ederson (Pauni 36milioni), Axel Witsel (Pauni 36milioni), Raul Jimenez (Pauni 34milioni), Nelson Semedo (Pauni 32milioni), Victor Lindelof (Pauni 31.5milioni) na Renato Sanches kwa Pauni 31.5milioni. Hapo hawajaorodheshwa mastaa kama Angel di Maria, Nemanja Matic na David Luiz.