Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Robertinho azungumzia ishu ya Ally Salim

Muktasari:

  • Wakati Salim akitupiwa lawama kipa huyo amechaguliwa mchezaji bora wa Simba kwa mwezi Aprili akiwapiku Jean Baleke na Kibu Denis.

Kocha Mkuu wa Simba amezungumzia suala la kipa, Ally Salum kufanya makosa katika mchezo na Namungo, Robertinho alisema sio muda wa kuanza kumtupia lawama bali anatakiwa kupongezwa kwa jitihada kubwa alizozionyesha hadi kufikia hapa.

"Salim ni kipa mzuri sana na kijana ambaye tunaamini ni tegemeo huko baadae sasa kitendo cha kumtupia lawama kwangu naona hakina mashiko bali tumpe moyo wa kujituma zaidi kwani hakuna mtu aliyekuwa sahihi,"

"Kwenye mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa na Wydad Casablanca hatua ya robo fainali, Clatous Chama na Shomari Kapombe walikosa penalti na ukiangalia ni wachezaji wakubwa sasa hakuna haja ya Wakati Salim akitupiwa lawama kipa huyo amechaguliwa mchezaji bora wa Simba kwa mwezi Aprili akiwapiku Jean Baleke na Kibu Denis.kurushiana lawama" amesema

Wakati Salim akitupiwa lawama kipa huyo amechaguliwa mchezaji bora wa Simba kwa mwezi Aprili akiwapiku Jean Baleke na Kibu Denis.

Salim zao la timu ya vijana ya Simba alipandishwa timu ya wakubwa miaka mitatu iliyopita, msimu huu ni kama anawasapraizi mashabiki wa timu hiyo kwa kuonekana langoni katika mechi mbili ikuwemo ile ya Dabi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 2-0.

Tangu kuumia kwa Manula, Salim amedaka michezo mitano ambapo mitatu ni ya Ligi Kuu Bara na miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.