Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Robertinho ataja mbinu mpya CAF

MSAFARA wa Simba unatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Guinea kwa ajili ya mchezo wa kwanza hatua ya makundi Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Horoya utakaochezwa Jumamosi hii.

Kocha wa Simba, Oliveira Robertinho amesema ubora ulioonyeshwa timu yake kucheza na kumiliki mpira pamoja na kupata ushindi ni kiwango kidogo kulingana na anachokitaka.

Robertinho alisema falsafa yake inataka kuona Simba inacheza soka la kasi kama ilivyo baadhi ya timu kutoka mataifa makubwa yaliyoendelea kisoka Afrika ya Morocco, Tunisia, Algeria na mengineyo yenye kucheza soka la kufanana na hilo.

Alisema ukiangalia timu zilizopo kwenye ligi kama Morocco zinacheza soka la kasi muda mwingi, zinamiliki mpira na mwisho wa siku zinafanikiwa kupata ushindi pamoja na mafanikio mengine makubwa.

“Ukiangalia klabu nyingi kutoka kwenye mataifa hayo zimekuwa hatari muda wote kwenye mechi za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), lakini hata ushindi kwenye ligi ya kwao na mashindano mengine huwa ni mkubwa,” alisema Robertinho na kuongeza:

“Nataka kuona Simba ikicheza soka la namna hiyo. Naamini tukiweza kufanya hivyo basi timu kutoka mataifa hayo tutakutana nazo kwenye mashindano ya CAF, tutaweza kushindana nazo vya kutosha nyumbani na ugenini tukapata matokeo mazuri dhidi yao.

“Tukifanikiwa kucheza soka la aina hiyo kama falsafa zangu, naamini hata tukikutana na timu nyingine zenye mafanikio kutoka nchi kama Afrika Kusini na DR Congo nazo tutakuwa bora dhidi yao kwenye maeneo mengi na kupata aina ya matokeo tunayoyahitaji.

“Kikosi cha Simba kina wachezaji zaidi ya 25 sio rahisi wote pamoja kuelewa kwa haraka kile ninachohitaji kutoka kwao kulingana na ninavyowaelekeza mazoezini, ila naamini taratibu kila kitu kitakuwa sawa.

Katika hatua nyingine Robertinho alisema Simba inakwenda kucheza dhidi ya Horoya kwa tahadhari kubwa kwani lengo ni kuanza vyema kwa kupata pointi ugenini ili kujirahisishia kazi kwenye michezo ya nyumbani.