Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prisons, Mtibwa Sugar hakuna mbabe

Muktasari:

  • Tanzania Prisons imeendelea kuwa na matokeo yasiyoridhisha kufuatia suluhu ya bila kufungana dhidi ya Mtibwa Sugar na kubaki mkiani kwa alama 13.

Mbeya. Uwanja wa Sokoine Mbeya umeendelea kuwa mgumu kwa Tanzania Prisons baada ya leo tena kushindwa kuutumia vyema kwa kuambulia suluhu ya bila kufungana dhidi ya Mtibwa Sugar.

Huo ulikuwa mchezo wa nne kwa timu hiyo kucheza uwanjani hapo ikiwa ni sare mbili ikiwamo dhidi ya Mbeya City na kupoteza miwili dhidi ya Polisi Tanzania na Ruvu Shooting chini ya Kocha wake, Patrick Odhiambo.

Katika mchezo wa leo Jumatano, Prisons walianza kwa kiasi wakishambulia zaidi lango la wapinzani ambapo dakika ya saba Jeremia Juma manusura aipatie bao lakini mpira wake uliomuacha Kipa Jeremia Kisubi haukuingia wavuni hadi beki, Frank George kuuwahi na kuuondosha eneo la hatari.

Mtibwa Sugar nao walijibu shambulizi, ambapo dakika ya 19, Mayanja Mululi shuti lake akiwa eneo zuri halikuweza kuzaa matunda baada ya kung'ang'ania kwenye tope kufuatia uwanja kuwa na majimaji na kufanya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Kipindi cha pili timu hizo zilifanya mabadiliko, ambapo Tanzania Prisons iliwatoa Lambart Sabiyanka na Dotto Shaban na kuwaingiza Samson Mbangula na Moses Kitandu, huku Mtibwa waliwapumzisha, Mayanja Mululi, Ismaili Mhesa, Nzigamasabo Styve na Nassoro Kiziwa na nafasi zao kujazwa na Boban Zirintunsya, Jafari Kibaya, Omary Hassan na George Makan'ga.

Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuwa faida yoyote kwa pande zote kuweza kupata ushindi na kufanya dakika 90 kumalizika kwa pande zote kuondoka na alama moja moja, ikiwa ni matokeo mabaya kwa Prisons kushindwa kung'atuka mkiani kwa kufikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi 17.

Pia matokeo hayo yanaifanya Mtibwa Sugar kuondoka jijini Mbeya kwa alama nne kufuatia ushindi wa mchezo wao na Mbeya Kwanza mabao 2-1 na kufikisha alama 16 katika msimamo wa Ligi Kuu.