Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prison pungufu yaikaba Yanga

Muktasari:

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 21, hivyo kuipa nafasi Simba yenye pointi 22, kuzidi kujichimbia kileleni iwapo itashinda kesho dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Dar/Mikoani. Yanga imelazimisha sare ya bao 1-1 na Prisons iliyocheza pungufu kwa zaidi ya dakika 50 baada ya mchezaji wake kupewa kadi nyekundu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 21, hivyo kuipa nafasi Simba yenye pointi 22, kuzidi kujichimbia kileleni iwapo itashinda kesho dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Yanga ilianza mchezo huo taratibu na kutoa nafasi kwa wageni Prisons kufunga bao la kuongoza dakika ya 10 lililofungwa na Eliuter Mpepo kwa shuti kali baada ya kumtoka beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante'.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Yanga na kulishambulia lango la Prisons, lakini safu ya ulinzi ya wajelajela hao iliyongozwa na nahodha Laurian Mpalile ilikuwa imara.
Prisons ilipata pigo dakika ya 36, baada ya  winga Lambert Sabiyanka kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kuonyesha nia ya kutaka kumpiga kiwiko beki wa Yanga Juma Abdul wakati wakiruka juu kuwania mpira.
Mwamuzi Shomari Lawi wa Kigoma hakujiuliza kutoka kadi nyekundu kwa Sabiyanka na kumuacha nahodha wa Prison, Mpalile akipiga magoti kusikitika na kuomba huruma ya mwamuzi.
Kadi hiyo iliwataoa mchezoni Prisons na kuwaruhusu Yanga kufika golini kwao na kupata bao la kusawazisha dakika ya 43 kwa kujifunga Jumanne Elfadhili akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Pius Buswite.
Katika mchezo huo Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa  Nadir Haroub 'Canavaro', Emmanuel Martin na Ibrahim Ajib na nafasi zao kuchukuliwa na  Kelvin Yondani, Geofrey Mwashiuya na Yusuph Mhilu wakati Prisons iliwatoa Salum Kimenya,r Mpepo na nafasi zao kuchukuliwa na  Hamis Maingo, Kazungu Mashauri na Fred Chudu mabaye baadae alitoka na kuingia  Kazungu Mashauri.

Kwenye Uwanja wa Namfua Singida wenyeji Singida United walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.
Mabao ya mataji wa Singida yalifungwa na Yusuph Kagoma dakika ya 17 na Danny Usengimana dakika ya 54.
Uwanja wa Mabatini Mlandizi, Ruvu Shooting waliichapa Majimaji mabao 2-1 wakati kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba, Kagera Sugar ilitoka suluhu na Stand United.
Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Mbao iliifunga  Mwadui bao 1-0. Bao la washindi lilifungwa na Emmanuel Mvyekure dakika ya 44.
 Simba vs Lipuli
Sare iliyopata Yanga leo inaweza ikawapa mzuka Simba wa kuifunga Lipuli kesho ili kuzidi kuwaacha mbali kwa pointi wapinzani wao.
Simba itaikaribisha Lipuli kwenye Uwanja wa Uhuru huku ikiwa na nafasi kubwa  ya kuzidi kujichimbia kileleni kwanim kama itashinda leo basi itafikisha pointi 25 na kuwazidi pointi nne mabingwa watetezi Yanga.
Imeandikwa na Oliver Albert, Eliya Solomon (Dar), Matereka Jalilu (Dodoma) na  Masoud Masasi (Mwanza).