Pluijm: Kila mtu ashinde mechi zake

Muktasari:

  • SBS na Azam FC wapo kwenye vita kali ya kuwania nafasi ya tatu baada ya timu hizo wiki hii moja imepoteza pointi zote tatu na nyingine ikiambulia moja ambayo imemfanya ajitofautishe kwenye msimamo kutokana na idadi ya pointi kuongezeka.

KICHAPO cha bao 1-0 walichokipata Azam FC kimemuibua Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Van Pluijm ambaye ameweka wazi kuwa sasa kila mmoja ashinde mechi zake mahesabu mwisho wa msimu.

SBS na Azam FC wapo kwenye vita kali ya kuwania nafasi ya tatu baada ya timu hizo wiki hii moja imepoteza pointi zote tatu na nyingine ikiambulia moja ambayo imemfanya ajitofautishe kwenye msimamo kutokana na idadi ya pointi kuongezeka.

Singida Big Stars ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 25 akishinda 14 sare tano na kufungwa tano imekusanya pointi 48, Azam FC imecheza mechi 25 imeshinda 14 sare tano na kufungwa tano imekusanya pointi 47 utofauti ni pointi moja.
Akizungumza na Mwanaspoti, Pluijm alisema mechi zilizobaki ndio zitaamua nani atamaliza nafasi ya tatu hivyo kila mmoja ashinde mechi zake ili kufikia malengo.

"Kufungwa kwa Azam FC kumepunguza presha kwa wachezaji wangu ambao walikuwa wanaamini sare yetu dhidi ya Coastal Union ingeweza kuongeza vita kubwa ya pointi tofauti na ilivyokuwa kwenye mabao ya kufunga na kufungwa;

"Tupo mbele kwa pointi moja ambayo haitupi kujiamini kwani Azam wakishinda mechi na sisi tukafungwa tunashushwa nafasi moja hivyo malengo ni kuhakikisha tunatumia nafasi kwenye kila mchezo uliobaki kwa kupata pointi zote tatu."

Alisema mechi zao tano walizobakiza zote zinaumuhimu wa kupata pointi tatu muhimu lakini sio kazi rahisi bila ya mbinu na mipango imara kuhakikisha wanafanikiwa huku akikiri kuwa timu anazokutana nazo pia zinahitaji matokeo.

"Tuna mchezo na Yanga inahitaji pointi kujihakikishia nafasi ya bkutwaa taji,tuna Polisi Tanzania ambaye yupo nafasi mbaya kwenye msimamo anapambana kusaka nafasi ya kubaki msimu ujao hivyo haitakuwa rahisi kwetu."


MECHI ZA SINGIDA
Singida BS v Polisi Tanzania
Singida BS v Yanga
KMC v Singida BS
Singida BS v Ruvu Shooting
Namungo v Singida BS

MECHI ZA AZAM
Azam v Mtibwa Sugar
Ruvu Shooting v Azam
Azam v Namungo
Coastal Union v Azam
Azam v Polisi Tanzania