Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukijichanganya kwa Simba umeumia!

Muktasari:

  • Rekodi hiyo ni ile ya kikosi hicho kuwa ndio wakali wa kuziponza timu pinzani kupata kadi nyingi nyekundu huku yenyewe ikinufaika kwa kupata penalti 13, ambazo ni nyingi kuliko timu yoyote kati ya 16 za Ligi Kuu.

SIMBA imefunika katika Ligi Kuu Bara. Licha ya kuwa ndio timu iliyovuna pointi nyingi nyumbani kupitia mechi 13 ilizocheza ikishinda 10 na kutoka sare mbili, ikipoteza moja, lakini kuna rekodi iliyoweka hadi sasa katika Ligi hiyo ambayo kama timu pinzani hazitakuwa makini zitazidi kuumia.

Rekodi hiyo ni ile ya kikosi hicho kuwa ndio wakali wa kuziponza timu pinzani kupata kadi nyingi nyekundu huku yenyewe ikinufaika kwa kupata penalti 13, ambazo ni nyingi kuliko timu yoyote kati ya 16 za Ligi Kuu.

Simba imeziponza timu pinzani kupata kadi nyekundu nne ikiwazidi vinara wa ligi hiyo Yanga walioziponza timu mbili tu, huku ikishikilia rekodi ya kuwa timu iliyovuna pointi nyingi ugenini, ikishika pia nafasi ya pili kwa zilizofanya vizuri nyumbani nyuma ya Simba.

Kadi nyekundu ya winga mshambuliaji wa Pamba Jiji, Hamad Majimengi aliyoonyeshwa katika kichapo cha timu hiyo cha mabao 5-1, Mei 8, 2025 katika mechi ya Ligi Kuu, kimeifanya Simba kuongoza kwa wapinzani wanaocheza nao hadi sasa msimu huu.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, mabao ya Simba yalifungwa na Jean Charles Ahoua aliyefunga ‘hat- trick’ na Leonel Ateba akitupia mawili, huku la kufutia machozi kwa Pamba Jiji likifungwa na Mathew Momanyi.

Simba ilimponza pia nyota wa maafande wa JKT Tanzania, Mohamed Bakari aliyelimwa kadi nyekundu Desemba 24, 2024 kwenye Uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam wakati Wekundu hao waliposhinda kwa bao 1-0, la penalti ya nyota Jean Charles Ahoua.

Kadi nyingine nyekundu iliyotolewa katika mechi ya Simba, ilikuwa ni ya kipa wa Fountain Gate, John Noble wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana bao 1-1, mechi ikipigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Manyara, Februari 6, 2025.

Kipa wa Mashujaa, Patrick Munthary akakutana na kadhia hiyo pia kwenye Uwanja wa KMC Complex, wakati kikosi hicho cha maafande kilipokutana na kichapo cha mabao 2-1, Mei 2, 2025, yaliyofungwa yote na Leonel Ateba kwa mikwaju ya penalti.

Katika mechi hiyo ambayo iligubikwa na matukio tata hali iliyosababisha kuongezwa kwa dakika 15, Mashujaa ilikuwa ni ya kwanza kupata bao la dakika ya tano, lililofungwa na mshambuliaji, Jaffary Kibaya.

Kwa upande wa Yanga katika mechi zake wapinzani wamepata kadi nyekundu mbili akianza Saleh Masoud wa Pamba Jiji wakati kikosi hicho cha Jangwani kikishinda mabao 4-0, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Oktoba 3, 2024.

Kadi nyingine nyekundu ni ya kipa wa JKT Tanzania, Denis Richard wakilala 2-0.

Katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Oktoba 22, 2024 mabao ya Yanga yalifungwa na Pacome Zouzoua na Clatous Chama

Rekodi zinaonyesha hadi sasa zimetolewa penalti 82, huku Simba ikiongeza kwa kupata 13, ikipoteza moja tu, huku 12 zikiwekwa kimiani na Leonel Ateba na Jean Ahoua kila mmoja akiwa na sita. Ateba ndiye aliyekosa penalti nyingine ya Simba, huku akiwa ndiye kinara wa kupiga mara nyingi akifanya hivyo mara saba.

Akizungumzia tukio la kadi nyekundu ya Majimengi, Kocha wa Pamba Jiji, Fredy Felix ‘Minziro’ alisema kinachochangia hali hiyo kutokea kwa mchezaji ni kutokana na kutoridhishwa na matokeo, au husababishwa pia kutokuwa sawa kimwili na kiakili.

“Mchezaji anaweza kufanya kila liwezekanalo lakini kila akijaribu anajikuta anafanya tofauti na matarajio yake, hali ya namna hiyo inamfanya kushindwa kumudu presha iliyopo na kusababisha kufanya makosa yanayoweza kumgharimu pia,” alisema.