Pitso Mosimane ataka timu nyingine ziige Yanga

Sunday June 26 2022
pitso pic
By Leonard Musikula

ALIYEKUWA kocha mkuu wa Al Ahly ya Misri na Mamelod Sondown ya Afrika Kusini, Pitso Mosimane naye avunja ukimya kwa kuwasifia Yanga kwa namna ambavyo wamelipokea Kombe la Ligi kuu.

Mosimane ameutumia mtandao wa Twitter kuipongeza Yanga huku akizishauri klabu zingine za Afrika kufanya kile ilichokifanya Yanga katika shughuli zao za kulipokea Kombe la Ligi.

"Hongera sana Yanga, Afrika pia inaweza kufanya gwaride lao la kombe kama timu za Ulaya.Tunahitaji kuona zaidi ya gwaride hizi kwa sababu inaonyesha upendo na shauku ya wafuasi wa soka la Afrika."

Advertisement