Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pistorius afuatwa jela

Muktasari:

  • Pistorious alimpiga risasi kadhaa mpenzi wake na kumuua nyumbani kwake, lakini alijitetea akisema hakukusudia kumuua kwani alidhani ni jambazi alimvamia

Serikali ya Afrika Kusini imeiomba Mahakama ya juu nchini humo kumwongezea kifungo mwanaridha mlemavu, Oscar Pistorius ‘Blade Runner’ aliyekutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp, Februari 2013.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Pretoria, Thokozile Masipa, alimhukumu Pistorius kifungo cha miaka sita baada ya kumtia hatiani kwa mauaji ya bila kukusudia, uamuzi ambao haujawaridhisha watu wengi.

Hivi karibuni, serikali hiyo kupitia Wakili, Andrea Johnson, ilirejea mahakamani na kuomba uamuzi wa Jaji Masipa ubatilishwe na mwanaridha huyo aliyejipatia umaarufu kwa kushiriki mbio akitumia miguu ya bandia kwa kuwa ni mlemavu, aongezewa muda zaidi wa kukaa jela.

“Jaji aliyeisikiliza kesi alikosa kabisa kuweka wazi sababu za kutotoa adhabu ya kifungo kisichopungua miaka 15 (Kwa mujibu wa sheria za Afrika Kusini) alipomhukumu Oscar Pistorious kwa mauaji ya Reeva Steenkamp,” wakili huyo aliiambia mahakama hiyo ambayo bado inaisikiliza rufaa hiyo.