Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Penalti yamtesa Sserunkuma

Straika Uganda aliyepiga penalti fyongo iliyoipa Tanzania Bara nafasi ya ubwete ya kutinga nusu fainali ya Cecafa Senior Challenge Cup, Danny Serunkuma, ameomba radhi kwa nchi yake.

Muktasari:

Danny ndiye aliyekosa penalti ya mwisho iliyoipa Stars ushindi wa penalti 3-2. Serunkuma ambaye hana rekodi ya kupoteza penalti, amesema kuwa hajiskii raha na itamgharimu.

STRAIKA wa Uganda aliyepiga penalti fyongo iliyoipa Tanzania Bara nafasi ya ubwete ya kutinga nusu fainali ya Cecafa Senior Challenge Cup, Danny Serunkuma, ameomba radhi kwa nchi yake.

Danny ndiye aliyekosa penalti ya mwisho iliyoipa Stars ushindi wa penalti 3-2. Serunkuma ambaye hana rekodi ya kupoteza penalti, amesema kuwa hajiskii raha na itamgharimu.

“Sijiskii raha, naomba radhi kwa mashabiki wa Uganda, haikuwa nia yangu kukosa ile penalti, kila mchezaji alitaka kufuzu hatua ya nusu fainali na kutetea ubingwa,” alisema.

“Ndio maana kwenye muda wa kawaida tulipambana sana, hii hali ya kukosa penalti inaniweka kwenye wakati mgumu lakini naomba mashabiki wanielewe.”

Waandishi wa Habari wa Uganda walioko mjini hapa wanadai kwamba walijua timu yao haitafika mbali kwa vile kikosi kilikuwa dhaifu na kilikuwa na wachezaji wawili tu wa maana ambao ni Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi. Uganda iliutema ubingwa huo katika mechi hiyo ya robo fainali huku wachezaji wakiwa hawaamini kilichotokea.

Tanzania Bara iliyosonga mbele kwa ushindi huo, leo Jumanne inacheza na wenyeji Kenya katika nusu fainali.