Pawasa alitabiri Simba inakufa 2-1 Kariakoo dabi

Muktasari:

  • Kabla ya mechi ya Kariakoo Dabi kupigwa jana Jumamosi Aprili 20, kuna wachezaji walitabiri matokeo ya nani ataibuka mbabe baina ya Yanga na Simba.

BEKI wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa, alipatia utabiri kwamba Yanga itashinda mechi ya Kariakoo Dabi ya jana kwa mabao 2-1. 

Kabla ya mechi ya Kariakoo Dabi kupigwa jana Jumamosi Aprili 20, kuna wachezaji walitabiri matokeo ya nani ataibuka mbabe baina ya Yanga na Simba.

Kati ya mastaa watano, wawili walipatia utabiri wao, ambao ni Charles Ilanfya wa Mtibwa Sugar na Pawasa, ambaye yeye alipatia hadi idadi ya mabao.

Ilanfya alitabiri Yanga kushinda, ila hakutaja mabao mangapi na alisisitiza haitakuwa na mabao mengi kama ilivyokuwa mzunguko wa kwanza ambao Simba ilipoteza kwa mabao 5-1.

Alitoa sababu ya utabiri wake akisema: "Yanga ipo vizuri kwa msimu huu, pamoja na hayo yote Simba haitakubali kupoteza kwa kipigo kikubwa tena, ingawa sijajua Wanajangwani watafunga mangapi."

Baada ya mechi Ilanfya amesema: "Ni kama Simba ilivyokuwa inachukua mataji kwa mfululizo, haikuwa na shaka ya kushinda mechi zake, ndio maana nilisema Yanga itashinda."

Pawasa kabla ya mchezo alisema: "Mechi inaweza ikamalizika kwa mabao 2-1, Simba haitakubali kipigo kikubwa na Yanga haina ubishi ipo vizuri kwa msimu huu."


WALIOCHEMKA

DANNY MRWANDA

Alitabiri 0-0 ama sare ya bao 1-1


BALAMA MAPINDUZI- MASHUJAA

Alitabiri sare ya mabao 2-2


RASHID JUMA - MTIBWA

Alitabiri 0-0 ama sare ambayo hakutaja mabao.