Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jangwani hapatoshi, Mbosso aipiga Aviola 

JANGWANI Pict

Muktasari:

  • Paredi hiyo ilianza mchana leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga walipokelewa kwa shangwe baada ya kurejea kutoka visiwani Zanzibar.

Ni shamrashamra, burudani na furaha ya aina yake katika makao makuu ya Klabu ya Yanga, ambapo mashabiki kwa maelfu wamefurika kusherehekea kilele cha paredi la mataji matano, ikiwa ni hitimisho la msimu wa mafanikio kwa timu yao.

Paredi hiyo ilianza mchana leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga walipokelewa kwa shangwe baada ya kurejea kutoka visiwani Zanzibar.

Kutoka hapo, msafara wa magari ya wazi ulianza ukielekea katikati ya jiji, ukiwa umeambatana na maelfu ya mashabiki waliokuwa barabarani.

Hatimaye, jioni hii, msafara umefika Jangwani mahali ambapo historia ya Yanga ilipo  na hapo ndipo burudani zimechukua nafasi yake rasmi.

Wakati hekaheka za burudani zikianza kivutio kikubwa ni msanii wa Bongo Fleva, Mbosso, ambaye amepewa jukumu maalum la kumaliza msimu kwa kishindo.

Mbosso amepanda jukwaani huku mashabiki wakimshangilia kwa nguvu, akiimba vibao vyake maarufu kama “Aviola”.  

“Aviola ni kwa ajili ya wapinzani waliobaki na ndoo ya plastiki. Leo tunasema, hii ndiyo Yanga ya mataji matano!” alisema mmoja wa mashabiki wakati wimbo huo.

Sherehe hizi zimesimamiwa kwa usalama wa askari  wa jeshi la polisi na walinzi binafsi wakihakikisha kila mmoja anafurahia bila bughudha.

Hadi kufikia saa 12:30  jioni, hakuna taarifa yoyote ya vurugu au changamoto ya kiusalama jambo linalothibitisha kuwa sherehe hizi zimeandaliwa vizuri.