Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamba yatoa dozi ya 5G Championship

Muktasari:

  • Baada ya ushindi huo timu hiyo inaendelea kujichimbia katika nafasi ya pili ikifikisha pointi 58 nyuma ya vinara Ken Gold wenye alama 60, huku kila timu ikibakiwa na michezo mitatu.

MATUMAINI ya Pamba Jiji kucheza Ligi Kuu msimu ujao yanazidi kuwa makubwa baada ya kutakata leo ikiibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Pamba imepata ushindi huo mkubwa msimu huu leo Machi 30, 2024 katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ukichezwa kuanzia saa 8:00 mchana na kuendelea kujichimbia katika nafasi ya pili kwenye Ligi ya Championship.

Ushindi wa mabao matano ni wa kwanza kwa Pamba msimu huu, ambapo imeshinda michezo miwili kwa mabao manne ikizichapa Cosmopolitan mabao 4-1 na Copco FC mabao 4-0.

Kwa ushindi huo, Pamba inafikisha pointi 58 zinazoifanya ibaki katika nafasi ya pili nyuma ya vinara Ken Gold wenye pointi 20, huku timu hizo zikibakiwa na michezo mitatu kila mmoja ambapo mbili za juu zitapanda moja kwa moja kwenda Ligi Kuu.

Katika mchezo huo ambao umehudhuriwa na mashabiki wengi na kuwa na amshaamsha za hapa na pale, Pamba imekwenda mapumziko ikiongoza mabao 2-1 ambayo yamefungwa na Michael Samamba dakika ya 14 na Issah Ngoah dakika ya 28, huku Polisi wakifunga bao kupitia kwa Taimur Makame dakika ya 38.

Kipindi cha pili, wenyeji wamerudi kwa kasi kubwa wakishambulia kwa nguvu na kupata mabao ya haraka kupitia kwa Ismaily Ally dakika ya 47, Daniel Joram dakika ya 58 huku bao la tano likipatikana dakika ya 89 baada ya beki wa Polisi Tanzania, Cliff Rumanyika kujifunga akijaribu kuokoa hatari langoni mwao.

Baada ya kushinda leo, Pamba imefikisha mchezo wa 12 katika Uwanja wa Nyamagana jijini hapa bila kupoteza, ikishinda 10 na sare mbili, huku mchezo pekee wa nyumbani iliyopoteza ilifungwa na Biashara United bao 1-0 mchezo ukipigwa mkoani Shinyanga katika Uwanja wa Mwadui.

Kocha Msaidizi wa Pamba Jiji, Renatus Shija amesema pamoja na wachezaji wake kucheza vyema lakini uchovu waliokuwa nao Polisi Tanzania ndiyo ambao umeibeba timu yake na kupata ushindi huo mnono kirahisi.

"Polisi wamefika jana saa 9 Alasiri hawakupata muda wa kupumzika nadhani fatiki yao sisi imetupa faida. Walimu wanahitaji wapate muda mrefu kuandaa timu zao," amesema Shija na kuongeza:

"Kwa hiyo viongozi wa timu zetu wawape makocha wa Kitanzania nafasi ya kuandaa timu zao na wawamini, inapotokea changamoto kama hizi hata kocha unashindwa kumlaumu anakuwa hana la kufanya."