Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome ajivunia kuitwa Afcon 2023

Muktasari:

  1. Pacome amejumuishwa kwenye kikosi hicho cha Tembo kitakachokwenda kushiriki fainali hizo zinazofanyika hapohapo nchini kwao.

BAADA ya kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua kujumishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa lake la Ivory Coast, kwanza ameishukuru Yanga kwa kumbeba.

Pacome amejumuishwa kwenye kikosi hicho cha Tembo kitakachokwenda kushiriki fainali hizo zinazofanyika hapohapo nchini kwao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Pacome alisema kutua kwake Yanga kumekuja na bahati kubwa kwani hakutarajia kama angepata habari njema kama hiyo ya kuichezea timu ya taifa hilo.

Pacome alisema ingawa amewahi kuzitumikia timu za taifa kwa vijana za taifa hilo lakini akasema haikuwa rahisi kama Yanga isingempa nafasi ya kuonyesha ubora wake.

Alisema kwasasa anajipanga kuhakikisha anaitumia nafasi hiyo kwa umakini ambapo anataka kwenda kufanya mambo makubwa endapo atabakizwa kwenye majina ya mwisho.

“Nilikuwa mchezaji bora wa ligi msimu uliopita kule Ivory Coast lakini sikupata bahati kama hii, ndani ya muda mfupi nikiwa hapa Yanga naitwa timu ya taifa hii ni bahati ya kucheza hapa,” alisema Pacome.