Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pablo awatisha Yanga Kirumba, asema lazima kieleweke

HAKUNA sare! Ni kauli ya kocha wa Simba, Pablo Franco akisisitiza kuichapa Yanga watakapokutana kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) huku Nasreddine Nabi akiweka msimamo.

Simba na Yanga zitaonyeshana ufundi kwenye nusu fainali ya ASFC, Mei 28 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza zikiwa na kumbukumbu ya kutoshana nguvu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kugawana pointi kwenye mechi zote mbili zilizopita za msimu huu.

Suluhu hizo mbili mfululizo msimu huu ni kama zimewachochea makocha hao ambapo yoyote atayeshinda atakutana na mshindi kati ya Coastal Union na Azam.

Simba itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 na kutwaa ubingwa wa ASFC dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma msimu uliopita zilipokutana kwenye fainali.

Pablo alisema kwamba; “Safari hii hakuna sare, mmoja lazima afungwe na mwingine afuzu kucheza fainali, nakwenda kuandaa kikosi bora zaidi cha ubingwa, lakini hatuwezi kufikia malengo hayo bila kushinda nusu fainali.”

“Sina shaka wachezaji wangu hawataniangusha, msimu huu tumecheza na Yanga michezo mitatu na yote hatujawafunga nadhani hilo si zuri kwa upande wetu tunataka kuweka rekodi nyingine ya ushindi katika mchezo huo wa nusu fainali,” alisema Pablo ambaye kikosi chake hakijaongoza msimamo wa Ligi tangu msimu huu uanze.

Katika mechi tatu za Dabi ya Kariakoo msimu huu, Simba ililala moja ya Ngao ya Jamii ya ufunguzi wa msimu kwa bao pekee la Fiston Mayele.

Pablo pia ana presha kubwa ya kutwaa taji hilo kwani tayari alikwama kufuzu nusufainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambalo ni moja ya malengo yake kimkataba.

Lakini Nasreddine Nabi yeye alijibu kwamba; “Tunahitaji kuwa mabingwa wa Ligi na wa FA, kwenye Ligi tayari tumetanguliza mguu mmoja, kwenye FA kazi ya kwanza ni kushinda nusu fainali.”

“Kisha tujipange kwa fainali, tunawaheshimu Simba kama timu kubwa, lakini hakuna namna nyingine zaidi ya kushinda mechi hiyo na nyingine zilizo mbele yetu ili kutimiza malengo ya klabu,” alisema Nabi huku mchambuzi msomi, Ally Mayay akisema mechi hiyo itaamuliwa na mbinu halisi za makocha. Alisema muunganiko wa Yanga na kuanza kurejea kwa safu ya usambuliaji ya Simba ni vitu ambavyo vitaongeza chachu ya upinzani kwenye dabi hiyo ya watani wa jadi.

“Simba kadri mechi zao zinavyokwenda ndivyo wanapafomu na kujiamini kwa wachezaji kunaongezeka, ni mechi ambayo timu zote zinaweza kupata matokeo mazuri kwa kufanya mashambulizi ya kutokea pembeni. Yanga sasa imefanikiwa kwenye eneo la kiungo, Simba yenyewe iko vizuri eneo hilo muda mrefu,” alisema Mayay.