Pablo alia na adhabu TFF

Kocha mkuu wa Simba, Pablo Franco leo ametema nyongo na kufukunga kuhusiana na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na kutozwa faini Sh3 milioni na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.
Adhabu hiyo ilitokana na kukataa kufanya mahojiano na wanahabari baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Mbeya City, Mtibwa Sugar sambamba na ule kati ya timu yake na Kagera Sugar ikiwa ni Sh1 milioni kwa kila mechi.
Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Biashara United hiyo kesho, Pablo anasema kuwa anashangzwa kwa adhabu hiyo aliopewa kwani anakumbuka kuwa ni mchezo mmoja tu ndio ambao hakuweza kuhudhuria mahojiano na waandishi wa habari na sio mitatu.
"Sikuhudhuria mahojiano baada ya mechi yetu na Geita Gold lakini nashangwa na kusikia kuwa sikuhudhuria pia na wa Kagera Sugar jambo ambalo sio sahihi kwani kwa kumbukumbu zangu ni kuwa siku hiyo hakukua na mahojiano baada ya mchezo kumalizika"anasema Pablo.
Pablo alifungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Sh500,000 kwa kosa la kupiga teke chombo maalumu cha kuhifadhia barafu/vinywaji baridi kwenye mchezo wa ligi namba 102, dhidi ya Mtibwa Sugar.
Katika taarifa hiyo ya TPLB imeeleza kuwa hiyo si mara ya kwanza kwa Pablo kufanya tukio la namna hiyo ambapo mara ya kwanza alipewa onyo baada ya kupiga teke kiti katika mchezo dhidi ya KMC uliopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.