Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oscar Oscar asimamisha shughuli TFF, asubiri uamuzi wa kamati

Oscar Oscar akizungumza na wandishi wa habari baada ya kurudisha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

Mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Oscar Oscar amesimamisha shughuli nje ya ofisi za TFF kwa dakika 35 alipokuwa akirejesha fomu.

Mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Oscar Oscar amesimamisha shughuli nje ya ofisi za TFF kwa dakika 35 alipokuwa akirejesha fomu.

Mgombea huyo ambaye anasubiri uamuzi wa kamati ya uchaguzi baada ya kukosa wadhamini kama kanuni inavyohitaji aliwasili TFF saa 7:40 mchana akiwa na msafara wa magari zaidi ya 10 na kuondoka saa 8:15 mchana.

Oscar Oscar akitoka kurudisha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Picha na Michael Matemanga

Baada ya kuwasili, Oscar aliyekuwa akiendeshwa alifunguliwa mlango wa gari na Majizo huku baadhi ya watu aliombatana nao wakiimba na kucheza na wengine wakimshangilia na kumuita rais, kisha akaingia ndani ya ofisi za TFF na wapambe wake wakisalia nje ya ofisi hizo wakiimba na kucheza.

Alipotoka, Oscar alisema amerejesha fomu lakini amekosa udhamini kama kanuni zinavyotaka kuwa na wagombea wasiopungua watano.

"Nimerudisha bila kuwa na udhamini hata mmoja, hivyo nasubiri uamuzi wa kamati," amesema Oscar.