Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oscar asema Hiddink atabaki Chelsea

Muktasari:

Hiddink amepoteza mechi moja tu kati ya 13 alizoinoa timu hiyo kabla ya mchezo wao wa jana Jumapili dhidi ya Manchester City kwenye Kombe la FA.


CHELSEA inaripotiwa kuhaha kusaka kocha mpya wa kumpokea, Guus Hiddink, mwishoni mwa msimu, lakini kiungo Mbrazili wa timu hiyo, Oscar, amefichua kwamba mastaa wote klabuni hapo wanataka Mdachi huyo abaki.

Hiddink amepoteza mechi moja tu kati ya 13 alizoinoa timu hiyo kabla ya mchezo wao wa jana Jumapili dhidi ya Manchester City kwenye Kombe la FA.

“Kwa kutazama namna Guus alivyofanya hadi sasa, ni vizuri akibaki. Timu imekuwa ikicheza vizuri sana, wachezaji wanajiamini na klabu imekuwa na furaha. Kuna uwezekano mkubwa atabaki,” alisema Oscar.

Oscar alisema Hiddink ni kama mjomba wao, kitu ambacho aliwahi kukisema pia kiungo wa Kidachi, Wesley Sneijder.

Oscar alisema: “Ni mtu safi sana, anacheka na siku zote amekuwa akitengeneza mazingira ya amani. Anahamasisha wachezaji na tumeanza kucheza vizuri, sawa tumetoa sare nyingi, zaidi hali ya kujiamini imerudi.”