Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Opare afungua njia Dodoma Jiji

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo Mghana, msimu uliopita ameitumikia timu ya Biashara United Mara iliyoshuka daraja, akihamishia makali yake Dodoma Jiji.

Dodoma. HATIMAYE Dodoma Jiji wametambulisha mchezaji wao wa kwanza waliyemsajili katika dirisha la usajili msimu huu, wakimtangaza mshambuliaji Collins Opare kutoka timu ya Biashara United.
Opare ambaye ni miongoni mwa washambuliaji waliomtungua kipa Djigui Diarra wa Yanga msimu ulioisha, amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo ya ''Walima Zabibu'' wa Dodoma.
Opare anakuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa katika wachezaji wapya waliosaini mkataba na wanaotarajiwa kusaini wakati wowote kuitumikia timu hiyo ambayo inajipanga kufanya vema msimu ujao wa mashindano tofauti na msimu ulioisha.
Miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kusajiliwa na timu hiyo na wanaosubiri kutangazwa ni Jimmy Shoji kutoka Mbeya Kwanza, Amaan Kyata kutoka Coastal Union, Hassan Mwaterema kutoka Kagera Sugar, Randy Bangala, Christian Ziggah na wengineo ambao wamefichwa.
Fredrick Mwakisambwe, Mwenyekiti wa kamati ya usajili alisema Opare ndio wameanza naye kama mchezaji wa kwanza katika wachezaji ambao wanamalizana nao kabla ya kuwaweka wazi na kuwataka mashabiki wa timu hiyo wasiwe na shaka.
''Mashabiki wetu wasiwe na shaka, huyu Opare ni miongoni mwa wachezaji tuliosema tunawasajili na bado wachezaji wengine zaidi wanafuata katika kuijenga upya timu yetu kwa msimu ujao wa ligi kuu na mashindano mengine'' alisema Mwakisambwe.