Onyango ni zaidi ya beki

Sunday August 22 2021
onyango pic
By Eliya Solomon

STRAIKA Mghana, Christain Zigah anayekipiga Biashara United amesema amekutana na mabeki mbalimbali katika Ligi Kuu Bara, lakini kwa Joash Onyango wa Simba alisema ni zaidi ya beki kwa namna anavyokaba uwanjani.

Zigah alisema alipomuona Onyango kabla ya mechi yao iliyopigwa Februari 18, mjini Musoma alimchukulia poa, lakini mziki aliokutana nao kwa beki huyo Mkenya ulimtoa jasho na timu yao kulala 1-0 kwa bao la Mghana mwenzake, Bernard Morrison.

“Ukiniuliza ni beki gani mkali niliyekutana naye katika Ligi nitakutajia Onyango, jamaa si wa kusimuliwa, nimekabiliana naye, nilijaribu kutumia mbinu zote, nilishindwa kumzidi ujanja,” alisema Zigah na kuongeza;

“Nilimchukulia pia kwa kuonekana kama ana umri mkubwa, hivyo niliamini asingenidhibiti lakini mambo yakawa tofauti kabisa, huyu jamaa ni zaidi ya beki.”

Advertisement