Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ole Solskjaer hasira tu, kisa vimeo vyake

Muktasari:

Ole aliwauliza wachezaji wake kama wanajali japo hata chembe tu ya kila kinachotokea kwenye timu hiyo kwa sasa, huku akisema kuna wachezaji hapo wanapaswa kuona aibu kwa sababu hawastahili kuvaa jezi za Man United.

MANCHESTER, ENGLAND.KOCHA Ole Gunnar Solskjaer amewaweka kikao wachezaji wake na kisha kuwauliza kama wanajisikia vizuri kutokana na kufanya ovyo kwa Manchester United.

Kocha huyo aliwaita wachezaji wake watu wa ovyo kabisa baada ya kushindwa kuwafunga Huddersfield kwenye Ligi Kuu England Jumapili iliyopita na hivyo timu hiyo kushindwa kutinga Top Four na kukwama kucheza UEFA msimu ujao.

Ole aliwauliza wachezaji wake kama wanajali japo hata chembe tu ya kila kinachotokea kwenye timu hiyo kwa sasa, huku akisema kuna wachezaji hapo wanapaswa kuona aibu kwa sababu hawastahili kuvaa jezi za Man United.

Kisha akawaambia kwa heshima ya mashabiki na klabu basi wahakikishe wanashinda mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya Cardiff utakaofanyika Jumapili. Kocha Solskjaer alikuwa mwenye hasira baada ya wachezaji wake kushindwa kuifunga timu ambayo ilishashuka daraja tangu wiki iliyopita.

Man United watamaliza msimu wao kwa kucheza dhidi ya timu nyingine iliyoshuka daraja huku wakifahamu wazi msimu ujao watacheza Europa League na si Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo wapinzani wao Liverpool wametinga fainali kwa msimu wa pili mfululizo.