Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Metacha aukubali mziki wa Mnigeria Singida

Muktasari:

  • Pamoja na kukosa nafasi ya kucheza mzunguko wa pili, Metacha amesema anatumia muda mwingi kufanya mazoezi na kujiweka fiti ili kujiandaa na msimu ujao.

KIPA wa Singida Black Stars, Metacha Mnata amesema  mzunguko wa kwanza ulikuwa bora kwake akipata nafasi ya kucheza tofauti na raundi ya pili ambayo panga pangua ni Obasogie Amas, raia wa Nigeria anayehusishwa huenda akatua Yanga 2025/26.

Pamoja na kukosa nafasi ya kucheza mzunguko wa pili, Metacha amesema anatumia muda mwingi kufanya mazoezi na kujiweka fiti ili kujiandaa na msimu ujao.

“Mpira wa miguu unahitaji uvumilivu na kujituma. Binafsi naona mzunguko wa kwanza nilifanya kazi nzuri na sasa ni zamu ya kipa mwenzangu, Amas, amepata nafasi na anaonyesha kiwango bora,” alisema Metacha ambaye hajaruhusu mabao katika mechi saba.

Alisema kwa jinsi alivyouona ushindani wa msimu huu unataka kujipanga kimazoezi ili ujao aweze kucheza kwa kiwango bora na kutegemewa katika timu.

“Japokuwa uwepo wa makipa wa kigeni umeongeza chachu naamini Tanzania ina makipa wenye vipaji vikubwa kama Yona Amos wa Pamba, Patrick Munthari wa Mashujaa pia bado naamini uwezo wa Aishi Manula licha ya msimu huu hakuwa mzuri kwa upande wake,” alisema.

Juu ya tetesi za Metacha huenda akajiunga na Azam, hakutaka kuzungumzia akisisitiza: “Mimi ni mchezaji timu yoyote inayohitaji huduma yangu tukikubaliana nitacheza.”