Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya City yampigia hesabu Maseke

Muktasari:

  • Maseke hadi sasa hajaruhusu bao katika mechi tatu na hakuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara, amekiri mkataba wake utaisha mwisho wa msimu huu, ingawa ameficha timu zinazomtaka.

KIPA Wilbol Maseke anayemaliza mkataba wake na KMC, anahusishwa kutakiwa na Mbeya City, ili kuongeza nguvu kwa ajili ya msimu ujao baada ya kupanda daraja, ikimaliza nafasi ya pili katika Ligi ya Championship.

Maseke hadi sasa hajaruhusu bao katika mechi tatu na hakuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara, amekiri mkataba wake utaisha mwisho wa msimu huu, ingawa ameficha timu zinazomtaka.

“Mimi ni mchezaji siwezi kukosa timu za kuchezea. Ni kweli mkataba wangu unaishia msimu huu, ila kabla ya kufanya uamuzi wa kukubaliana na ofa za timu nyingine nitaisikiliza kwanza KMC,” alisema.

“Ligi ni ngumu inatakiwa kujipanga, ingawa sikuwa na msimu mzuri wa kucheza kikosini haijanifanya nikate tamaa ya kuendelea kupambana na kujiweka fiti.” Kipa huyo aliyewahi pia kukipiga Azam FC alisema kutokana na uzoefu alionao wa kucheza Ligi Kuu hawezi kusumbuliwa na vipindi vya mchezaji kupanda na kushuka.

“Nilicheza Azam liyokuwa na ushindani mkali, nikaja KMC nikafanikiwa kufanya vizuri msimu wa kwanza, ndiyo maana najiamini msimu ujao nitafanya vizuri.”