Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ofisa Habari Fountain Gate atua DTB

Timu ya  DTB inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza leo imemtambulisha rasmi aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa timu ya Fountain Gate, Juma Ayo baada ya kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja.

Mratibu wa DTB FC, Muhibu Kanu alisema kuwa wameamua kumpa Ayo idara hiyo nyeti wakiamini atakuwa chachu katika kuiunganisha timu hiyo na wapenzi na mashabiki wa soka nchini.

"Juma Ayo ni mwandishi wa habari mbobevu na mwenye uzoefu wa kuhudumu katika nafasi hiyo hivyo uwepo wake tunaamini utasaidia kuipa chati timu yetu na kuiweka karibu zaidi na Watanzania ambao wengi wanatamani kuona tukipanda Ligi Kuu ambalo ndilo lengo letu kubwa," alisema Kanu.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutambulishwa, Juma Ayo alisema atahakikisha anatoa mchango wake ili timu hiyo iweze kupanda Ligi Kuu.

"DTB ni timu yenye malengo na hata usajili ambao imefanya unaonesha wazi kwamba una uongozi ambao unafahamu na kujua nini unakifanya hivyo kwangu mimi hili ni jambo kubwa na naahidi nitajitolea kadri niweze kuhakikisha lengo la msingi ambalo ni kupanda daraja linatimia," alisema Ayo.

Msimu uliopita, Juma Ayo alikuwa Ofisa Habari wa Fountain Gate Academy ambayo nayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ambayo aliitumikia kwa muda wa mwaka mmoja.