Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtaka, Tandau kuchuana urais TOC

TOC Pict

Muktasari:

  • Wagombea 28 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi huo ikiwamo wanne wanaowania urais, watatu nafasi ya makamu wa rais na na 21 wanaowania nafasi tano za ujumbe.

MAKUBALIANO ya pamoja kati ya Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC), Serikali ya Tanzania na uongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) yamewarejesha wagombea wanne akiwemo Anthony Mtaka, waliokuwa wameenguliwa kuwania uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa TOC.

Wagombea 28 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi huo ikiwamo wanne wanaowania urais, watatu nafasi ya makamu wa rais na na 21 wanaowania nafasi tano za ujumbe.

Kurejeshwa kwa  Mtaka  ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Njombe kunakoleza mchuano mkali  kwenye nafasi ya urais inayowania pia na makamu wa rais wa TOC anayemaliza muda wake, Henry Tandau, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leonard Thadeo na Hassan Khairalla Tawakal kutoka Zanzibar.

Wengine waliokuwa wameenguliwa katika usaili na sasa wamerejeshwa ni Rahim Kalyango na Suleiman Mahmoud Jabir (naibu katibu mkuu anayemaliza muda wake) wanaowania nafasi ya makamu wa rais na Donald Massawe anayewania ujumbe ambao awali Kamisheni ya uchaguzi huo iliwaengua

Rais wa TOC, Gulam Rashid  amesema makubaliano ya IOC, TOC na Serikali  yalifanyika baada ya sintofahamu ya mara kwa mara uchaguzi huo ukiahirishwa mara kadhaa tangu mwaka 2024.

"Katika makubaliano hayo tulikubaliana pia wale wagombea wanne waliokuwa wameenguliwa katika mchakato wa usaili awali kurejeshwa," amesema Gulam.

Awali katibu mkuu wa TOC,  Filbert Bayi alisema baada ya makubaliano sasa uchaguzi utafanyika Julai 5, 2026 katika Hoteli ya Peacock, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Amesema wapiga kura kwenye uchaguzi huo wako 42 ambapo 39 ni wajumbe kutoka vyama vya michezo nchini na watatu wanatoka Kamisheni ya Wachezaji ya TOC.