Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota wa Ligi Kuu waiteka Ngorongoro Heroes

Muktasari:

Kocha huyo ameita kikosi hicho kinajiandaa na michezo ya kufuzu kwa Olimpiki 2020

Dar es Salaam. Kocha wa timu ya taifa ya vijana wenye umri usiozidi miaka 23 'Ngorongoro Heroes', Kim Poulsen ameita wachezaji wengi wanaocheza Ligi Kuu katika kikosi chake kinachojiandaa na michezo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan 2020.

Katika kikosi hicho cha wachezaji 35, idadi kubwa ya nyota walioitwa ni wale wanaochezea timu za Ligi Kuu wale waliozaliwa kuanzia mwaka 1997 huku wawili wakitoka katika Ligi Daraja la Kwanza na wengine wawili wakitokea Zanzibar.

Timu zilizotoa wachezaji wengi katika kikosi hicho ni Azam wachezaji watano, Simba  (1), Yanga (4), Mbeya City (3),  Majimaji (2), Singida United (2), Stand United (2) na Mwadui (2).

Timu nyingine zilitoa wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Ruvu Shooting, Prisons, Miembeni City, Njombe Mji, JKU, Mwadui, Mtibwa, Ndanda na Ashanti United.

Kocha msaidizi wa Ngorongoro Heroes, Oscar Milambo alisema wameita kikosi hicho wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

"Bbenchi la ufundi tumejiridhisha kiwango cha hawa wachezaji baada ya kuwafuatilia kwa ukaribu katika timu zao ambazo idadi kubwa zipo Ligi Kuu.

Mkakati wetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zilizo mbele ya kuwania kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo, Japan 2020.

Wachezaji walioitwa ni: Metacha Mnata, Joseph Prosper, Masoud Abdallah, Abbas Kapombe na YahyYahya Zayd (Azam FC), Cleotas Sospeter, Yusuph Mhilu, Emmanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya (Yanga), Ismail Aidan, Salum Kihimbwa na Hassan Mganga (Mtibwa) na Eliud Ambokile, Emmanuel Kakuti na Medson Mwakatundu (Mbeya City).

Wengine ni Liza Mafwea na Bakari Kijuji (Prisons), Adam Salamba na Stanley Angeso (Stand United), Award Salum na Agaton Mapunda (Njombe Mji), Omary Mponda, Ayoub Masoud na Baraka Majogoro (Ndanda FC), Salum Chuku na Yusuph Kagoma (Singida United), Derushi Shaliboko (Ashanti United), Awesu Ally (Mwadui), Mohammed Jailan (Miembeni City), Yusuph Mlipili (Simba), Faisal Salum (JKU), Joseph Ilunda (JKT Ruvu), Idrissa Mohammed (Majimaji) na William John (Ruvu Shooting).