Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Tabora United amzimia Mpanzu

Muktasari:

  • Mpanzu alijiunga na Simba dirisha dogo la usajili na tayari ameanza kuonyesha ubora katika kikosi hicho akiingia moja kwa moja kikosi cha kwanza amecheza dakika 786 mabao matatu na asisti tatu.

BEKI wa zamani wa Polisi Tanzania na Yanga anayekipiga kwa sasa Tabora United, Yassin Mustafa amemtaja Elie Mpanzu, ndiye winga hatari zaidi katika Ligi Kuu Bara na ni Luis Miquissone mpya wa kikosi cha Simba.

Mpanzu alijiunga na Simba dirisha dogo la usajili na tayari ameanza kuonyesha ubora katika kikosi hicho akiingia moja kwa moja kikosi cha kwanza amecheza dakika 786 mabao matatu na asisti tatu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Yassin alisema mchezaji anayeweza kucheza nafasi mbili hadi tatu eneo la ushambuliaji ni hatari, akisisitiza ni suala la muda mchezaji huyo kukubalika lakini kwa wadau wanaoujua mpira mchezaji ukimuona siku moja tu unamuelewa.

“Mpanzu ni mzuri kila eneo analopewa nafasi ya kucheza, anaweza kucheza kulia na kushoto, pia hata namba 10 ni mchezaji ambaye anaweza kufanya mambo makubwa Simba,” alisema Yassin na kuongeza;

“Ana kasi, nguvu na akili ya mpira sio rahisi kukabana na mchezaji wa aina yake ukitumia nguvu navutiwa na aina ya uchezaji wake nafikiri anaweza akawa amekuja kuziba pengo la Miquissone ambaye ameacha alama katika ligi yetu kutokana na balaa alilolifanya.”

Yassin alisema ligi ya Tanzania inakua msimu hadi msimu na kuvuta mastaa wengi wakubwa kuja kuicheza jambo analomini ni fursa kwao kujiongeza kwa kujifunza kupitia nyota wa kigeni na kutoa changamoto ya ushindani.

Akizungumzia Tabora Utd, alisema timu hiyo sasa inapitia upepo mbaya lakini wao kama wachezaji wanafanya majukumu yao kama wanavyopangiwa na benchi la ufundi huku akiahidi kuwa watakuwa bora kwenye mechi za mwisho ili kuhakikisha wanamaliza tano bora.

“Unajua hata sisi hatuelewi nini kinatokea kwa sababu timu ilianza msimu vizuri mzunguko wa pili mambo ni magumu kupoteza mechi tano mfululizo hakuna mchezaji ambaye anafurahia hilo tumekaa na benchi la ufundi kujua shida iko wapi naamini mechi zinazofuata tutakuwa bora na hatutarajii kung’oka nafasi tuliyopo.”