Nuh Mziwanda amlilia mwanaye

Muktasari:

Ni yule aliyezaa na mke wake wa ndoa ambaye inaelezwa mama wa mtoto huyo tayari ameanzisha maisha na mume mwingine.

Wakati bado akiendelea kukimbiza na ngoma yake ya Bao la Ushindi, Nuh Mziwanda bado mara kadhaa ameendelea kutoa mapovu kwa aliyekuwa mke wake, Nawaal ambaye waliachana na inasemekana mpenzi wake huyo alikwenda kuolewa na mwanaume mwingine.

Nuh Mziwanda ameendelea kulalamika hasa kuhusu mtoto wake ambaye anasema kuwa anamkumbuka sana.

"Nakumiss sana mwanangu Anya yaani Mungu anajua jinsi gani moyo wangu unaenda mbio nikikumbuka au ukinijia akilini maana najua haufurahi kama ungekuwa na uwepo wangui karibu. Najua hauhisi upendo kama uliokuwa unahisi kipindi upo karibu yangu napenda ningekukuza kwenye misingi yangu sheria zangu na kanuni zangu kama Baba yako. Mama yako hakutendei haki kabisa…

Nimelia sana juu yako ila sasa namkabidhi Mungu hili suala na naamini atakulinda atakupa tabasamu sahihi japo upo mbali na mimi,Nakupenda Anyaghile wangu," aliandika.