Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Niyonzima kuchezesha droo ya Kagame

Muktasari:

  • Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 24 hadi Agosti 7 mwaka huu nchini Rwanda, itashirikisha timu 12 ambazo ni bingwa mtetezi Singida Black Stars na Simba kutoka Tanzania. Zingine ni KVZ (Zanzibar), APR na Rayon Sports za Rwanda, Vipers (Uganda), Al Hilal na El Merriekh (Sudan), Gor Mahia (Kenya), Mogadishu City (Somalia), Jamus (Sudan Kusini), FC Garde Républicaine (Djibouti).

KIUNGO wa zamani wa Simba na Yanga pamoja na timu ya taifa ya  Rwanda, Haruna Niyonzima, anatarajiwa kuhusika katika uchezeshaji wa droo ya michuano Kagame inayotarajiwa kufanyika Ijumaa ya Julai 10, 2026 mjini Kigali nchini Rwanda.

Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 24 hadi Agosti 7 mwaka huu nchini Rwanda, itashirikisha timu 12 ambazo ni bingwa mtetezi Singida Black Stars na Simba kutoka Tanzania. Zingine ni KVZ (Zanzibar), APR na Rayon Sports za Rwanda, Vipers (Uganda), Al Hilal na El Merriekh (Sudan), Gor Mahia (Kenya), Mogadishu City (Somalia), Jamus (Sudan Kusini), FC Garde Républicaine (Djibouti).

Droo hiyo itafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Amahoro kuanzia saa 4:00 asubuhi, ikiwa ni maandalizi ya mashindano hayo yatakayochezwa kwenye viwanja vya Kigali Pele na Amahoro.

Jumla ya timu 12 zitapangwa katika makundi matatu, huku kila kundi likiwa na timu nne. Kinara wa kila kundi pamoja na timu moja bora iliyomaliza nafasi ya pili ndizo zitakazofuzu hatua ya nusu fainali.

Meneja wa Mashindano wa CECAFA, Yusuf Mossi, alisema mfumo huo utazifanya timu zipambane tangu hatua ya makundi kwa kuwa nafasi za kufuzu ni chache.

Alieleza kuwa, mashindano hayo yatakuwa sehemu muhimu ya maandalizi kwa klabu zinazotarajiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2026-2027, itakayoanza Septemba mwaka huu.

CECAFA imethibitisha rasmi ushiriki wa Singida Black Stars katika mashindano hayo ikiwa ni bingwa mtetezi baada ya msimu uliopita kuifunga Al Hilal ya Sudan kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Dar es Salaam.

Kwa Simba, huu utakuwa ni mwendelezo wa kurejea kwenye michuano hiyo ya ukanda wa CECAFA baada ya kukosekana kwa miaka saba. Wekundu hao wa Msimbazi ndio klabu yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Kagame Cup, wakiwa wameutwaa ubingwa mara sita.

Mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ushiriki wa baadhi ya mabingwa na vigogo wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku yakitumika kama kipimo muhimu kuelekea msimu mpya wa mashindano ya kimataifa ya CAF.

Awali Singida BS walikuwa wakidaiwa kuwa huenda wasishiriki kutokana na kutopewa zawadi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo msimu uliopita ambapo no dola 30,000 ambazo ni zaidi ya Sh78 milioni

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Singida BS, Hussein Masanza, alisema: “Tutatumia mashindano hayo kama sehemu ya maandalizi ya msimu ujao, tunaamini kuwa suala letu litapatiwa ufumbuzi.”